SAYANSI STANDARD FOUR REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

Jina la mwanafunzi ________________________
Namba ya upimaji____________________

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE

 S09 SAYANSI 

 

 Muda: Saa 1 Mwaka: 2025 

 Maelekezo kwa mtahiniwa 

  1. Mtihani huu una sehemu A na B zenye jumla ya maswali sita (6)
  2. Jibu maswali yote kama ulivyoelekezwa katika kila sehemu.
  3. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa katika mtihani.
  4. Epuka kufuta kufuta.
  5. Simu za mkononi, karatasi zisizohusika na vitabu haviruhusiwi kaika chumba cha mtihani.
  6. Kumbuka kuandika namba yako ya mtihani, mkoa, wilaya na shule katika kila ukurasa kwenye sehemu uliyopewa upende wa juu kulia.
 KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU 
 NAMBA YA SWALI   ALAMA   SAHIHI YA MTAHINI 
 1.  
 
 2.  

 3.  

 4.  

 5.  

 6.  

 JUMLA 

 SEHEMU A: (ALAMA 22) 

 Jibu maswali yote katika sehemu hii. 

1. Chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu sahihi kwenye kisanduku kwa kila kipengele (i)-(v)

(i) Tawi lipi la sayansi linahusika na elimu ya wanyama?

  1. Kemia
  2. Bailojia
  3. Fizikia
  4. Jiografia  [    ] 

(ii) Ipi kati ya zifuatazo sio kanuni ya afya?

  1. Kufanya mazoezi
  2. Kula mlo kamili
  3. Kupata muda wa kupumzisha mwili na akili
  4. Kunywa pombe kali kiasi kidogo tu  [    ] 

(iii) Kundi gani la vyakula kati ya haya yafuatayo hutupatia protini?

  1. Karang ana maji
  2. Samaki na mihogo
  3. Nyanya na karafuu
  4. Samaki na maziwa  [    ] 

(iv) Ugonjwa unaoenezwa na mbu jike anayeitwa anaofelesi ni upi?

  1. Malaria
  2. UKIMWI
  3. UVIKO-19
  4. Tetekuwanga [    ] 

(v) Barafu ni aina gani ya maada?

  1. Gesi
  2. Yabisi
  3. Kimiminika
  4. Gesi na yabisi  [    ] 

2. Oanisha maneno kutoka Orodha A na yale ya Orodha B kisha andika herufi ya jibu katika sehemu uliyopewa.

 Orodha A   Jibu   Orodha B 
(i) Maji [    ] 
  1. Kitu chote huungua
  2. Hayana rangi.
  3. Vitu vinavyohitajika katika uunguaji.
  4. Baadhi ya sifa za viumbe hai
  5. Hutusaidia kukua
  6. Hutusaidia kujua ukweli wa mambo.
(ii) Joto, Oksijeni, Fueli [    ] 
(iii) Uunguaji kamili [    ] 
(iv) Kula, kupumua, Kukua [    ] 
(v) Uchunguzi na majaribio ya kisayansi [    ] 

3. Chagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku.

  Viumbe hai na visivyo hai, lava, tunutu, hatua nne, wadudu, chura, nyoka, viumbe wanaoishi

(i) Metamofosisi kamili ____________________________________________ 

(ii) Hatua ya kwanza ya ukuaji wa nzi ________________________________

(iii) Baada ya miezi mitatu hubadilika na kuwa mende kamili ______________________

(iv) Makundi makuu ya viumbe _______________________________________

(v) Mnyama aina ya amfibia ________________________________

(vi) Nzi, panzi, mende na mbu___________________________________

 SEHEMU B: (ALAMA 28) 

 Jibu maswali yote kutoka sehemu hii. 

4. Kamilisha hatua za uchunguzi wa kisayansi kwa kuzipa namba hatua zifuatazo kuanzia 1 hadi 8. Namba 1 na 2 imeshajazwa kama mfano.

 Hatua ya uchunguzi 

 Namba katika mpangilio (Hatua ya ngapi?) 

(i) Kubaini tatizo

1

(ii) Kubuni dhanio

2

(iii)Kuchambua data


(iv) Kuandika taarifa.


(v) Kuandaa mahitaji ya jaribio


(vi) Kutafsiri matokeo


(vii) Kufanya jaribio na kukusanya data


(viii) Hitimisho


5.  Angalia picha zifuatazo kwa makini kisha jibu maswali yanayofuata.

Maswali

(a) Picha A, B, C, na D zinawakilisha aina gani ya nishati?

_____________________________________________________________________________________

(b) Ni herufi gani katika picha inaonesha chanzo cha asili cha nishati uliyoitaja hapo juu (a)?

_____________________________________________________________________________________

(c) Taja chanzo kisicho cha asili cha nishati uliyoitaja hapo juu (a) unachokiona pichani.

_____________________________________________________________________________________

(d) Picha E na F zinawakilisha aina gani ya nishati?

_____________________________________________________________________________________

(e) Herufi E ni jiko la aina gani?

_____________________________________________________________________________________

(f) Herufi F ni jiko la aina gani?

_____________________________________________________________________________________

6. (a) Taja vifaa viwili vya TEHAMA unavyovifahamu.

(i) ______________________________________________________________________________________

(ii) ______________________________________________________________________________________ 

(b) Andika manufaa mawili ya kutumia vifaa vya TEHAMA ulivyovitaja.

(i) ________________________________________________________________________________________

(ii) _______________________________________________________________________________________

STANDARD FOUR SAYANSI EXAM SERIES 53  

STANDARD FOUR SAYANSI EXAM SERIES 53  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS - TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MAGU

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA IV TAREHE 23 NA 24 AGOST 2023

SAYANSI NA TEKNOLOJIA

MUDA: SAA 1:30 AGOST 2023

MAELEKEZO

  1. Mtihani una maswali matano yenye vipengele vya namba za kirumi
  2. Jibu maswali yote
  3. Andika majina yako kwa usahihi kwenye kila ukurasa

1. Chagua jibu sahihi na ujaze kwenye viboma

i. Mazingira machafu yanavutia imagevya magonjwa

A: Vijidudu B: Ndege  C: Watu D: Maji [     ]

ii. Kutupa taka ovyo, uchomaji wa taka ovyo ni vitendo vinavyosababisha uharibifu wa image

A: Mashamba B: Udongo C: Mazingira D: Vyoo [     ]

iii. Jane ni kiongozi wa darasa na alitoa tangazo. Je, alitumia aina gani ya nishati? image

A: Mwanga B: Jua C: Sauti D: Umeme [     ]

iv. Maji yanaweza kubadilika katika hali tatu za maada ambazo ni image 

A: Yabisi, gesi na jiwe

B: Yabisi, barafu na gesi C: Jiwe, hewa na kimiminika D: Yabisi, gesi na kimiminika [     ]

v. Kiwango cha jotoridi la 100°C au 212°F ni pale maji yanapofikia kuchemka. kitendo hicho huitwa image

A: Kizingiti cha mgando wa maji  B: Kizingiti cha mchemko wa maji

C: Kizingiti cha myeyuko wa maji  D: Kizingiti cha mvuke wa maji [     ]

2. Oanisha maneno kutoka kifungo A na kifungo B ili kuakamilisha sentensi

KIFUNGU A

MAJIBU

KIFUNGU B

i. Kipindupindu


A. Kufanya mazoezi

ii. Malaria


B. Kunawa mikono baada na kabla ya kula

iii. Taifodi


C. Kuchemsha maji ya kunywa, chakula kifunikwe vizuri

iv. Kifua kikuu


D. Kushiriki michezo

v. Ukimwi


E. Kupuliza dawa ya kuua wadudu na kuondoa maji yaliyotuama



F. Kutofanya ngono au kubaki na mmoja

3.Tumia maneno yafuatayo yaliyo kwenye jedwali kujibu maswali yafuatayo

Kubainisha tatizo, cherehani, friza, vimeng'enyo, jokofu, chanjo,dhanio

i. Kifaa kinachotunika kutunza chakula na vinywaji huitwa image

ii. Hatua ya kwanza katika kufanya uchunguzi wa kisanyansi inaitwa? image

iii. Kinga isiyo ya asili huitwa image

 iv. Kemikali zinazosaidia usagaji wa chakula tumboni huitwa? 

v. image ni mashine tata


4. Soma kifungu kifuatacho cha habari kisha jibu maswali yafuatayo.

Maji ni maada ya asili ipo katika hali ya kimiminika. Kikemia maji huundwa na hydrojeni na oksjeni. Maji huchukua 70% ya uso wa dunia ikiwemo mito, maziwa na bahari, ardhi huchukua sehemu ya asilimia inayobakia. Vyanzo vya asili vya maji ni mvua, chemichemi, visima na bahari. Maji ya asili hayawezi kuwa safi na salama kabisa.

Maji ni maada inayobadilika kwenda yabisi, gesi na kimiminika, tena kupitia njia mbalimbali. Maada yabisi ya maji ni barafu na mvuke ni maji katika hali ya gesi. Joto la maji likipanda husababisha mvukizo wa maji lakini joto likishuka husababisha maji kuganda.

MASWALI

i. Maji yakichemshwa huunda nini? image

ii. Je, maji kikemia huundwa na nini? image

iii. Je, ni kipi husababisha maji kubadilika kutoka maada moja kwenda nyingine? image

iv. Taja chanzo kimojawpo cha asili cha maji kilichotajwa kwenye habari uliyoisomaimage


v. Ni asilimia ngapi ya uso wa dunia huchukua sehemu isiyo na maji? image

5. Tumia mchoro huu wa simu kujibu maswali uliyopewa


i. Herufi A inawakilisha image

ii. Herufi B inaonyesha image

iii. Herufi C inaonyesha image

iv. Kitufe cha kupiga na kupokea simu kinaonesha na herufi gani? image

v. Kazi ya kifaa kilichoonyesha hapo ni image

STANDARD FOUR SAYANSI EXAM SERIES 33  

STANDARD FOUR SAYANSI EXAM SERIES 33  

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

UPIMAJI WA UTAMILIFU DARASA LA NNE

MKOA WA NJOMBE

SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Muda: Saa 1:30 Mwaka :2023

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A na B zenye jumla ya maswali Sita (6).
  2. Jibu maswali yote.
  3. Majibu yote yaandikwe katika nafasi zilizotolewa katika kila swali.
  4. Andika majibu yote kwa kutumia kalamu ya wino wa bluu au mweusi.
  5. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha upimaji.
  6. Andika Jina na Namba yako ya Upimaji katika sehemu ya juu kulia ya kila ukurasa.
KWA MATUMIZI YA UPIMAJI TU
 NAMBA YA SWALI   ALAMA   SAINI YA MPIMAJI
1

2

3

4

5

JUMLA

SAINI YA MHAKIKI


SEHEMU A:-

Chagua herufi ya jibu sahihi

1. i. Mwili wa binadamu una viungo ambavyo hufanya kazi tofauti, kipi kati ya viungo vifuatavyo hufanya kazi ya kuhisi? _________________

  1. pua
  2. masikio
  3. ngozi
  4. macho [       ]

ii. Viumbe hai wana sifa mbalimbali, kitendo cha kiumbe hai kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine huitwa_____________

  1. kujongea
  2. kukua
  3. kizaliana
  4. kutoa takamwili [       ]

iii. Babu alikuwa anaota moto ili kujihifadhi dhidi ya baridi. Je nishati ya joto ilimfikia babu kwa njia ya_______________________________

  1. mpitisho
  2. msafara
  3. mgusano
  4. mnururisho [       ]

iv. Amina alipima urefu na upana wa darasa, ambapo alipata hatua sita urefu na upana hatua tatu. Ni aina ipi ya vipimo alitumia?_____

  1. vipimo rasmi
  2. vipimo visivyo rasmi
  3. vipimo kamili
  4. vipimo vya urefu [       ]

v. Mama aliweka maziwa kwenye jokofu jana jioni ili yagande lakini mpaka kufikia asubuhi yalikuwa hayajaganga. Ni sehemu ipi maziwa yaliwekwa kwenye jokofu _______

  1. Friji
  2. Friza
  3. Hita
  4. Ovena [       ]

2. Oanisha fungu A na lile B ili lkuleta maana iliyo sahihi na uandike herufi ya jibu sahihi katika nafasi zilizoachwa wazi.

Fungu A

Fungu B

i. Utumbo mwembamba

A. Betri

ii. Utumbo mpana

B. Kusharabu chakula

iii. Usanifishaji

C. Kusharabu kwa maji na madini

iv. Asiyoona

D. Ukosefu wa vitamin

v.

E. Kitendo cha mmea kujitengenezea chakula chake.

Fungu A

(i)

(ii)

(iii)

(iv)

v

Fungu B.






SEHEMU B

Tumia maneno yaliyopo kwenye jedwali kujaza nafasi zilizo wazi

Jua, kabohaidreti, kucheka na kulia, Protini, mpitisho

3. (i) Chakula cha kujenga na kukuza mwili____________________________

(ii) Binadamu hutoa sauti kwa njia ya_______________________________

(iii) Chanzo kikuu cha nishati duniani ni ______________________________

(iv) Joto husafiri katika waya na maada ngumu kwa njia ya______________

(v) Chakula cha kuupa mwili nguvu_________________________________

SEHEMU C

4. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata

Maji ni maada ya asili, ipo katika hali ya kimiminika. Kikemia maji huundwa na haidrojeni na oksijeni. Maji huchukua 75% ya uso wa dunia ikiwemo mito, maziwa na bahari, ardhi huchukua sehemu ya asilimia inayobakia. Vyanzo vya asili vya maji ni mvua, chemichemi, kisima na bahari. Maji ya asili hayawezi kuwa safi kabisa. Maji ni maada inayobadilka kwenda yabisi na gesi na kimiminika tena kupitia njia mbalimbali. Maada yabisi ya maji ni barafu na mvuke ni maji katika hali ya gesi. Joto la maji likipanda husababisha mvukizo wa maji lakini joto likishuka husababisha maji kuganda

MASWALI

i. Je, ni asilimia ngapi huchukua sehemu isio na maji?_________________

ii. Vyanzo vya asili vya maji ni __________________ na _______________

iii. Je, ni kipi husababisha maji kubadilika kutoka maada moja kwenye nyingine?___________________________________________________

iv. Maji kikemikali huundwa na_________________ na ________________

v. Maji yakichemka huunda_______________________________________

Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kujaza jibu sahihi

5. i. Jotoridi la maji likifikia kiwango cha nyuzi joti sentigredi 100 ni sawa na farenhaiti___________________________________________________

ii. Msaada unaotolewa kwa mtu aliyeumia au kuugua ghafla kabla ya kumpeleka hospitali huitwa_____________________________________

iii. Miale ya mwanga inapotoka midia moja kwenda midia nyingine angavu_____________________________________________________

iv. Kifaa kinachotumika kuhifadhi vitu mbalimbali katika hali ya ubaridi ili visiharibike huitwa____________________________________________

v. __________________________ni vipimo vinavyokubalika katika jamii na havitofautiani mahali popote vinapotumika________________________

SEHEMU D :

6. Chunguza mchoro ufuatao kisha jibu maswali yafuatayo

(i) A ni ______________________________________________________

(ii) B ni ______________________________________________________

(iii) C ni ______________________________________________________

(iv) D ni ______________________________________________________

(v) E ni ______________________________________________________


STANDARD FOUR SAYANSI EXAM SERIES 23  

STANDARD FOUR SAYANSI EXAM SERIES 23  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

MTIHANI WA UPIMAJI DARASA LA NNE

SAYANSI

SEHEMU A

1.Chagua herufi ya jibu sahihi kisha uandike katika kisanduku

(i)Sifa mojawapo ya kiumbe hai ni ……………

(A)Kujificha(B)Kukua (C)Kucheza(D)Kulia (     )

(ii)Kati ya wadudu wafuatao ni yupi ana sumu kali……………….

(A)Kipepeo(B)Mende(C)Nge(D)Popo (     )

(iii)Kuna aina …………………….za mende 

(A)Mbili(B)Tatu (C)Nne(D)Moja (     )

(iv)Kipi ni cahakula cha wanga kati ya hivi?

(A)Ugali(B)Mtindi(C)Mayai (D) Pilau (     )

(v)Sifa mojawapo ya mwanga ni………………………..

(A)Kuzimika(B)Kumilika(C)Kuasfiri katika mstari mnyoofu (D)Kuwaka (     )

2.Jibu vipengele(i ) hadi (v) kwa kuoanisha maelezo katika kifungu A na dhana katika kifungu B.Andika majibu sahihi kwenye sehemu ya majibu uliyopewa


KIFUNGU A

JIBU


KIFUNGU B

i

Jua


A

Umbo lenye giza linatokea baada ya mwanga kuzuiwa na kitu

ii

Kivuli


B

Chanzo cha asili cha mwanga

iii

Mstari mnyoofu


C

Matokeo ya mwanga kuakisiwa

iv

Akisi


D

Miale ya mwanga kurudishwa baada ya kutua kwenye uso unaong’aa

v

Taswira


E

Namna ambavyo miale ya mwanga inavyosafiri




F

Nyota na mwezi

3.Jibu kipengele ( i) hadi (v) kwa kuchagua neno sahihi kutoka kwenye kisanduku ulichopewa na uliandike neno hilo kwenye nafasi husika

Uchafuzi wa hewa,utunzaji wa mazingira,nishati,tabia za mwanga,ujelezaji

(i)Husafiri katika mstari mnyoofu,kuakisiwa na kupinda……………………………..

(ii)Mwanga,joto,umeme,na sauti ni………………………………………………………………

(iii)Hali ya kuchakata takataka ili kutengeneza vitu vingine huitwa ………………………………..

(iv)Kufanya usafi wa mazingira,kupanda miti na kutocchoma misitu moto ni……………………………….

(v)Moshi kutoka viwandani,magari,chakavu na mitambo ya viwandani husababisha…………………………

SEHEMU B

4.Soma kwa makini habari uliyopewa kisha jibu maswali yanayofuata

Mwezi uliopita tulitembelewa shuleni na mtaala wa kilimo kutoka wilayani.Mtaalamu huyu wa kilimo alitufundisha vitendo vinavyosababisha uharibifu wa udingo katika mazingira yanayotuzunguka.Mtaalamu huyu alitueleza kwamba uharibifu wa udongo unasababishwa na shughuli za binadamu za kila siku,shughuli hizo ni mfano wa takataka ambazo si rafiki kwa udongo ni kama vile mifuko ya plastiki,makopo,chupa za plastiki na misumari

Athari za utupaji takataka hovyo husababisha kuwepo kwa mazalia ya vijidudu vya magonjwa kama vile maralia,sambamba na hilo pia hupelelekea maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na homa ya matumbo.

Hivyo basi ili kuondoa tatizo hilo la uchafuzi wa udongo hatuna budi kukusanya takataka na kuziweka kwenye pipa kisha kuzitupa sehemu mahali salama au kuzichoma kwenye tanuri maalumu lililombali na makazi ya watu ili kuepusha uchafuzi wa hewa.

MASWALI

  1. Ni nini kinasababisha uharibifu wa udaongo…………………,………………….
  2. Ni magonjwa gani yapi ya mlipuko husababishwa na uchafuzi wa udongo?..................na……………………….
  3. Kwa nini unashauriwa kchoma takataka mbali na makazi ya watu?________________________________
  4. Ni wapi tunashauriwa kuweka takataka baada ya kazi kufanya na kabla ya kwenda kutupa sehemu salama_______________.
  5. Taja mifano miwili ya takataka ambazo si rafiki kwa udongo_________________ na _______________________

5. Chunguza mchoro ufuatao kisha jibu maswali yanayofuata.


MASWALI.

  1. Herufi A inawakilisha ______________________________
  2. Herufi B inawakilisha ______________________________
  3. Herufi C inawakilisha ______________________________
  4. Herufi D inawakilisha ______________________________
  5. Taja jina la mchoro huo ______________________________


STANDARD FOUR SAYANSI EXAM SERIES 11  

STANDARD FOUR SAYANSI EXAM SERIES 11  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256