HISTORIA STANDARD FOUR REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

Jina la mwanafunzi ________________________
Namba ya upimaji____________________
Mkoa____________________________
Halmashauri___________________

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

 HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI 

MTIHANI WA UPIMAJI  DARASA LA NNE 

 A07   HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI  

 Muda: Saa 1 Mwaka: 2025 

 Maelekezo kwa mtahiniwa 

  1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali sita(6)
  2. Jibu maswali yote kama ulivyoelekezwa katika kila sehemu.
  3. Majibu yote yaandikwe kwenye nafasi ulizopewa katika mtihani.
  4. Epuka kufuta kufuta.
  5. Simu za mkononi, karatasi zisizohusika na vitabu haviruhusiwi kaika chumba cha mtihani.
  6. Kumbuka kuandika jina lako, namba ya upimaji, mkoa na halmashauri kila ukurasa kwenye sehemu uliyopewa upende wa juu kulia.
 KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU 
 NAMBA YA SWALI   ALAMA   SAHIHI YA MTAHINI 
 1.  
 
 2.  

 3.  

 4.  

 5.  

 6.  

 JUMLA 

  SEHEMU A: (ALAMA 20)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake kwenye kisanduku kwa kila kipengele (i)-(x)

(i) Hali ya kupiga hatua mbele au kuongeza kitu kutoka kiwango cha chini kwenda cha juu huitwaje? 

  1. Ujima
  2. Ukabaila
  3. Umwinyi
  4. Maendeleo

(ii) Mifano ipi inaeleza stadi za elimu kabla ya ukoloni?

  1. Uhunzi, ususi na uporaji
  2. Ufugaji, uvuvi na ujenzi
  3. Ususi, ufugaji na uvuvi
  4. Kilimo, uvuvi na ujangili

(iii) Kwanini elimu wakati kabla ya ukoloni ilitolewa kwa lugha ya jamii husika?

  1. Kupinga ukoloni
  2. Kujua vitu vya muhimu pekee
  3. Kuelewa maarifa kwa urahisi
  4. Kuwaficha watoto wasijue yanayoendelea

(iv) Shughuli ya ususi ilichangiaje maendeleo ya jamii kabla ya ukoloni?

  1. Kuhifadhi mazao na vyombo
  2. Kupata utajiri
  3. Kuonesha ufahari
  4. Kupata sifa kwa watu

(v) Teknolojia ya chuma ilisaidia vipi maendeleo ya kilimo?

  1. Zana za chuma zilirahisisha kilimo
  2. Chuma ilitumika kama zawadi kwa wakulima
  3. Chuma ilikuwa inalimwa
  4. Chuma ilipelekea wakulima na wafugaji wagombane

(vi) Katika utunzaji wa mazingira, jamii iliweka sheria gani ili kutunza mazingira kabla ya ukoloni?

  1. Kutowinda wanyama na kukata miti ovyo
  2. Kulima karibu na vyanzo vya maji
  3. Kulisha wanyama ovyo kwenye vyanzo vya maji
  4. Kukata miti sana

(vii) Miongoni mwa maadili yaliyokuwa yanazingatiwa kwa wataalamu wa sayansi asilia kabla ya ukoloni ilikuwa ni___

  1. Kuwapa zawadi kila muda
  2. Kuwaheshimu na kuwajali
  3. Kuwa karibu nao mara kwa mara
  4. Kuwa nao mbali

(viii) Jamii ipi kati ya hizi ilitengeneza mavazi kwa kutumia magome ya miti na ngozi za wanyama?

  1. Wahaya
  2. Wazaramo
  3. Wapare
  4. Wazigua

(ix) Eneo maarufu kwa kilimo cha umwagiliaji kabla ya ukoloni ni lipi kati ya haya?

  1. Umatumbi
  2. Engaruka
  3. Kilwa kivinje
  4. Olduvai

(x) Ni teknolojia ipi ya asili ya kuhifadhi samaki ilikuwa ikitumika hapo kale?

  1. Friji
  2. Kemikali maalum
  3. Kukausha kwa moto na kuweka chumvi
  4. Kuchemsha sana na kutia Magadi mengi

2. Oanisha maneno kutoka Orodha A na yale ya Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi kwenye sehemu uliyopewa.

Orodha A

Majibu

Orodha B

(i) Dini [    ]
  1. Maziwa, mabwawa na mito.
  2. Kuabudu katika miti mikubwa na mapango.
  3. Ukatili kwa watoto.
  4. Wajibu wa mtoto
  5. Upendo na chuki
  6. Vitendo vya heshima
  7. Kutoamini uwepo wa mizimu.
(ii) Kupewa kazi kinyume na umri wako [    ]
(iii) Shughuli za uvuvi [    ]
(iv) Kusaidia kazi ndogo ndogo za nyumbani [    ]
(v) Kusalimia na kuongea lugha nzuri [    ]

3. Chagua jibu kutoka kwenye kisanduku kisha liandike kwenye nafasi zilizoachwa wazi.

  China, Litti, Mkwawa, Mirambo, Mangi sana, Machemba, Ushujaa wa vita, Ujerumani

(i) Chifu wa jamii za wahehe kabla ya ukoloni ___________________________________

(ii) Mtemi wa jamii za wanyaturu kabla ya ukoloni _______________________________

(iii) Mtemi wa wanyamwezi kabla ya ukoloni ___________________________________

(iv) Njia mojawapo ya kupata uongozi hapo kale_______________________________

(v) Jamii nyingi zilipambana na wavamizi kutoka wapi?__________________________

SEHEMU B: (ALAMA 18)

Jibu maswali yote kutoka sehemu hii.

4. Soma mchoro ufuatao kisha jibu maswali yanayofuata.

image

Maswali

(a) Mchoro huo hapo juu unawakilisha nini?

_________________________________________________________________

(b) Kiongozi gani wa shule anahakikisha wanafunzi wanafuata sheria za shule?

_________________________________________________________________

 (c) Ni ngazi ipi inahusika kuhakikisha wanafunzi wenzao wanafuata sheria za shule?

_________________________________________________________________

(d) Ni nani anahakikisha darasa lake linakuwa na maadili?

_________________________________________________________________

5. Soma picha ifuatayo kisha jibu maswali.

image

Maswali

(i) Vitu unavyoviona pichani kwa jina moja huitwaje?

______________________________________________________

(ii) Ni wageni kutoka maeneo gani walileta vitu hivyo pichani?

______________________________________________________

(iii) Nini matumizi ya vitu hivyo?

______________________________________________________ 

(iv) Ni aina gani ya urithi unaoonekana pichani?______________________________________________________

(v) Ni urithi gani mwingine ulioletwa na watu walioleta vitu vinavyoonekana hapo pichani?

______________________________________________________

SEHEMU: (ALAMA 12)

Jibu swali la sita (6) 

6. Sentensi zifuatazo zimechanganywa haziko katika mtiririko wenye kuleta mantiki. Zipange sentensi hizo kwa kuzipa herufi A-F ili kupata habari yenye kuleta mantiki kuhusu familia.

(i) Uhusiano huo ni wa asili kwani mtu hujikuta tu yupo katika familia fulani na watu fulani.

(ii) Baada ya mtu kuwa na ndugu hao, anapaswa atambue kuwa baba na mama ni viongozi wa familia.

(iii) Vile vile, anapaswa kujua na kutambua mchango wa kila mwanafamilia ili kuwa na familia yenye upendo.

(iv) Familia ni uhusiano wa damu uliopo baina ya watu fulani.

(v) Hivyo anapaswa awaheshimu na kuwajali kwa kila hali kwani ni sababu ya yeye kupatikana. 

(vi) Katika kujikuta huko, mtu huwa ana baba, mama, kaka na dada zake katika familia husika.

STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 50  

STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 50  

Jina la Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Shule . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS UTAWALA WA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

MKOA WA DODOMA 

MTIHANI WA MUHULA DARASA LA NNE

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI [06E]

MUDA : Saa 1:30 2025

MAELEKEZO:

  1. Mtihani huu una maswali sita (6) yenye sehemu A na B
  2. Jibu maswali yote kwenye sehemu zote
  3. Andika majibu yote katika nafasi ulizopewa
  4. Majibu yote lazima yaandikwe kwa kutumia kalamu ya wino mweusi au bluu.
  5. Simu za mkononi au nyenzo yoyote hairuhusiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika jina na namba ya mtihani katika kila ukurasa wa mtihani huu.
KWA MATUMIZI YA WATAHINI TU
Namba ya Swali Alama Sahihi ya Mtahini Sahihi ya Mhakiki
1.


2.


3.


4.


5.


6.


JUMLA


SEHEMU A: (ALAMA 26)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi kisha ujaze kwenye kisanduku ulichopewa

i. Kitendo cha kutoa au kupokea kitu chochote kwa lengo la kupewa upendeleo katika jambo fulani au kupata huduma fulani huitwaje? [      ]

A. Zawadi C. Nidhamu B. Rushwa D. Msaada

ii. Tanzania ni nchi iliyoundwa na mataifa mawili; Tanganyika na Zanzibar. Ni lini muungano wan chi hizo ulifanyika?

A. 9/12/1961 C. 14/10/1999 B. 26/12/1964 D. 26/4/1964

iii. Ipi miongoni mwa tabia zifuatazo huonyesha kitendo cha heshima?

  1. Kumpisha mkubwa kukalia kiti kwenye gari 
  2. Kukataa kuagizwa na mkubwa wako 
  3. Kucheza na wanyama
  4. Kutumia lugha mbaya

iv. Katika historia ya Tanzania, Ni mreno gani wa kwanza kuingia pwani ya Afrika Mashariki?

  1. Mwl. J.K. Nyerere 
  2. Dr. Louis Leakey 
  3. Vasco da Gama
  4. Sultan Seyyid Said

v. Kitu chochote ambacho mtu anastahili kupewa huitwaje?

A. Haki C. Mali B. Wajibu D. Majukumu

2. Oanisha maelezo yaliyopo kwenye orodha A na majibu yaliyopo kwenye orodha B, na kisha uandike herufi ya jibu sahihi kwenye chumba ulichopewa.

ORODHA A MAJIBU ORODHA B
(i) Majengo ya zamani yaliyobaki kama sehemu ya historia na utamaduni.
  1. Makavanzi
  2. Makumbusho
  3. Masimulizi
  4. Maeneo ya kiakiolojia
  5. Magofu

(ii) Sehemu ambapo nyaraka na taarifa mbalimbali za kihistoria huhifadhiwa.
(iii) Maeneo yanapopatikana masalia ya mambo ya kale na utamaduni wa mwanadamu.
(iv) Maeneo yanayotumiwa kuhifadhi vitu vyenye historia na urithi wa kiasili na kiutamaduni.

3. Chagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku kasha jibu maswali yanayofuata;

Kaole, Zanzibar, Olduvai Gerge, Zinjanthropus, Link

(i) Mji palipogundulika mabaki ya Dinosaria wa Tendaguru.

image

(ii) Sehemu ambapo lipo jengo la maajabu ambalo lina historia ya kuwa jengo la kwanza kuwekwa lifti za umeme.

image

(iii) Eneo lilipogunduliwa fuvu la Binadamu wa kale na Dr. Louis Leakey.

image

(iv) Jina lilopewa fuvu la binadamu wa kale lililogunduliwa mwaka 1959.

image

(v) Mji yanapopatikana magofu ya msikiti na kituo cha kuhifadhia watumwa.

image

SEHEMU B: (ALAMA 24)

4.  Ainisha matendo yafuatayo kwa kusoma maelezo yake na kuweka alama ya vema (√) katika chumba sahihi. Kipengele cha tano (v) kimefanywa kama mfano kwa ajili yako.

Kitendo

Kitendo cha kimaadili

Kitendo kisicho cha kimaadili

(i) Kupigana na wenzako



(ii) Kusalimia watu wakubwa



(iii) Kushirikiana na watu wengine



(iv) Kuwatukana watu wazima



(v) Kumsaidia mzee kubeba mizigo


5.  Tazama picha hizi kwa makini kasha jibu maswali yanayofuata

Maswali

i. Mwanamke aliyeoneshwa katika picha A anafanya nini?

image

ii. Mwanaume anayeonekana kwenye picha B anafanya nini?

image

iii. Jamii ya mtu aliyeoneshwa kwenye picha B hupendelea kula chakula gani.

image

iv. Aina ya nguo aliyoivaa mtu aliyeoneshwa kwenye picha B inaitwaje?

image

6. Soma habari ifuatayo kasha ujibu maswali yanayofuata;

Jamii za Tanzania hapo Kale zilifanya biashara na wafanyabiashara kutoka Mashariki ya Mbali na ya Kati. Nchi hizo ni India, Irani, Iraki, Kuwait, China na Saud Arabia. Biashara hii ilifanyika katika miji iliyopo katika mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi kama vile Dar es Salaam, Bagamoyo, Tanga, Kilwa na Zanzibar. Biashara hizi zilifanyika kwa kubadilishana bidhaa. Bidhaa kubwa katika biashara hii kutoka nchini ilikuwa dhahabu na pembe za ndovu. Dhahabu ilitoka Zimbabwe kupitia bandari ya Sofala, Msumbiji. Kutoka kwa wageni kuja nchini, bidhaa kubwa zilikuwa shanga na vyombo vya ndani kama vile mabakuli na sahani za udongo. Baadhi ya mabaki ya bidhaa hizi yapo katika Makumbusho hapa nchini, kama vile makumbusho ndogo iliyopo Kaole, Bagamoyo.

Maswali

(i) Mabaki ya bidhaa zilizotumika katika biashara na watu wa Mashariki ya mbali zimehifadhiwa wapi?

image

(ii) Taja bidhaa mbili zilizokuwa zinaletwa kutoka kwa wageni?

image

(iii) Tja nchi mbili za Mashariki ya mbali zilizotajwa kwenye habari hii?

image

(iv) Taja miji miwili iliyopo katika Mwambao wa Pwani

image


STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 48  

STANDARD FOUR HISTORIA EXAM SERIES 48  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256