JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI NUSU MUHULA KIDATO CHA KWANZA MACHI 2026
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
MUDA : MASAA 2: 00
MAELEZO
SEHEMU A ( Maksi 15)
1. Chagua jibu lililo sahihi zaidi kwa kipengele cha (i)- (x).
i. Somo la historia ya Tanzania na maadili hufundisha kuhusu mwenendo wa shughuli za kiuchumi kama kilimo, utalii, uvuvi na ufugaji. Hii inaonyesha uhusiano wake na somo gani?
ii. Wabantu ni jamii yenye idadi kubwa zaidi ya watu hapa Tanzania tofauti na jamii nyingine. Asili ya jamii ni wapi?
iii. Kama wewe ni mgeni katika jamii mojawapo ya kitanzania, utajuaje kama jamii unayoishi nayo ni jamii ya wakushito?
iv. Jengo la ngome kongwe linalopatikana chake chake katika kisiwa cha pemba lilijengwa na waarabu wa Omani katika karne ya ?
v. Bonde la olduvai lina umuhimu gani katika urithi wa kihistoria ya jamii ya Tanzania?
vi. Wahadimu ni neno lenye Asili ya ..............
vii. Utafti wa kihistoria unaonesha kuwa chimbuko la wamasai ni wapi?
viii . Mojawapo ya matokeo ya kuhamia kwa wabantu katika maeneo ya afrika mashariki na hasa Tanzania ni mabadiliko katika utamaduni wa jamii za asili. Jambo gani ni uthibitisho wa mabadiliko haya?
ix.ISMAT ni mtoto mwenye maadili mazuri awapo nyumbani na shuleni.Ni tabia gani hatutegemei kuona kwa ISMAT
x. kiongoz wa jadi wa jamii ya watumbatu alijukana kwa jina la......
2 .Oanisha maelezo ya jamii katika orodha A na jamii husika katika orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi
| KUNDI A | KUNDI B |
| I . Jamii ya watu waliosambaa afrika kabla ya mtawanyiko wa wabantu wanaotumia lugha ya kugongagonga ulimi II. Jamii kubwa inayowa husisha waadimu wanaopatikana katika eneo la kati na kusini mwa kisiwa cha unguja III.Jamii kubwa yenye mchanganyiko wa waafrika na waasia waliohamia Tanzania kutokea Somalia miaka1000 Iliyopita IV. Kundi la watanzania ambalo ni jamii ya wafugaji waliohamia kutokea kusini mwa Sudani V. Mfano wa jamii ya kitanzania inayoishi katika mkoa wa manyara na mkoa wa Arusha, kusini mwa Ngorongoro |
|
SEHEMU B (55 MAKSI)
JIBU MASWALI YOTE KATIKA SEHEMU HII
3(a). Eleza maana ya Jamii
(b).Historia inaonesha kuwa kutoka enzi,watu wameishi pamoja na kudumisha upendo ,amani , na mshikamano katika jamii. Kwa mujibu wanafalsafa na wanazuoni ulio wasoma ,eleza namna walivotoa fasili tofauti tofauti za dhana ya jamii
4.(a).Jamii huishi katika vijiji , miji , nchi na mataifa kupitia shughuli kama vile uwindaji,kilimo,u vuvi na biashara .Bainisha na fafanua makundi yanayo unda jamii
(b).Fafanua sababu (tano) zilizo Fanya jamii za kitanzania kuishi pamoja toka zama za kale.
5.Taja na ufafanue hatua mbalimbali za mabadiliko ya kimaendeleo ambazo jamii za kitanzania zimeishi na kupitia
6.(a).Eleza maana ya historia ya Tanzania na maadili
(b).Taja vyanzo vitatu vya historia ya Tanzania na maadili
(c).Bainisha changamoto (nne) za kukuza Maadili katika Jamii unamoishi.
7.Fafanua malengo ya ujenzi wa Maadili katika Jamii za asili za kitanzani .
8.(a).Eleza maana ya wabantu ni nini....?
(b).Taja sababu zilizo wafanya wabantu kutawanyika na kuingia Afrika mashariki
SEHEMU C ( 30 MAKSI)
9.Andika insha isiyozidi maneno mia Moja (100).Eleza umuhimu wa somo la historia ya Tanzania na Maadili .
10.Eleza uhusiano uliopo kati ya somo la historia ya Tanzania na maadili na masomo yafuatayo
FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 246
FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 246
MTIHANI WA ROBO MUHULA WA KIDATO CHA KWANZA
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
MUDA: SAA 2:30 MWAKA: 2026
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika kipengele (i) mpaka cha (x) kisha andika herufi ya jibu sahihi katika sehemu ya karatasi ya mtihani uliyopewa
i. Somo la Historia ya Tanzania na Maadili linajumuisha dhana kuu ngapi?
ii. Historia inahusu mambo gani?
iii. Ni kwa nini ni muhimu kujua historia yetu?
iv. Mabadiliko gani yamekuwa yakizingatiwa katika historia ya Tanzania?
v. Maadili ni nini?
vi. Maadili yana umuhimu gani kwa taifa?
vii. Somo la Historia ya Tanzania na Maadili linatusaidiaje?
viii. Ni nini umuhimu wa somo la Historia ya Tanzania na Maadili?
ix. Somo la Historia ya Tanzania na Maadili linahusiana na masomo gani mengine?
x. Ni kwa nini maadili ni muhimu katika jamii?
MAJIBU
| i | ii | Iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
2. Oanisha SAFU A kwa kutoa jibu sahihi kutoka katika SAFU B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika visanduku chini yake.
| SAFU A | SAFU B |
|
|
MAJIBU
| I | ii | iii | iv | v |
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Eleza ni kwa jinsi gani uhamiaji umechangia katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi katika jamii za Kitanzania?
i. ______________________________________________________________________
ii. ________________________________________________________________________
iii. ________________________________________________________________________
iv. ________________________________________________________________________
v. ________________________________________________________________________
4. Tanzania ina takribani makabila mia moja na ishirini na kila kabila lina utamaduni wake wa asili pamoja na mila na desturi zake . Taja makabila manne makuu yanayopatikana Tanzania, na utaje asili ya kila kabila.
i. ________________________________________________________________________
ii. ________________________________________________________________________
iii. ________________________________________________________________________
iv. ________________________________________________________________________
v. ________________________________________________________________________
5. Watanzania wengi katika jamii ya leo tumetokana na wabantu kwani lugha nyingi za makabila nchini Tanzania hufanana matamshi pia hata maana. Eleza kwa kutoa mifano mitano (05) shughuli za kiuchumi na kijamii za jamii za Kibantu.
i. ________________________________________________________________________
ii. ________________________________________________________________________
iii. ________________________________________________________________________
iv. ________________________________________________________________________
v. ________________________________________________________________________
6. Kwa kutoa mifano dhabiti eleza uhusiano kati ya somo la Historia ya Tanzania na Maadili na masomo mengine kama vile
i) Jiografia ________________________________________________________________________ ________________________________________________________________________
________________________________________________________________________
ii)Hisabati. ________________________________________________________________________ ________________________________________________________________________
________________________________________________________________________
7. Taja baadhi ya mambo yanayozingatiwa katika historia ya Tanzania.
i. __________________________________________________________________
ii. __________________________________________________________________
iii. __________________________________________________________________
iv. __________________________________________________________________
v. __________________________________________________________________
8. Jamii huusisha watu wa sehemu tofauti tofauti kwakulijua hilo, wewe ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza fafanua dhana ya jamii na vipengele vyake.
i. __________________________________________________________________
ii. __________________________________________________________________
iii. __________________________________________________________________
iv. __________________________________________________________________
v. __________________________________________________________________
9. a) Nini maana ya maadili
________________________________________________________________________ ________________________________________________________________________
________________________________________________________________________
b) Toa faida (04) nne za maadili katika taifa la Tanzania
i. __________________________________________________________________
ii. __________________________________________________________________
iii. __________________________________________________________________
iv. __________________________________________________________________
SEHEMU C (Alama 15)
Jibu swali namba 10
10. Shule ya Sekondari ‘’KATWE’’ kulikua na mgongano baina ya wanafunzi wa kidato cha kwanza ‘’a’’ wakidai kwamba somo la historia ya Tanzania na maadili halina faida kwao huku kidato cha kwanza ‘’b’’ hawajui somo linahusu nini kabisa. Wewe ukiwa kama mtaalamu wa historia na maswala ya utamaduni wasaidie wanafunzi wa kidato cha kwanza ‘’a’’ na ‘’b’’ katika shule ya ‘’KATWE’’ kujua umuhimu wa somo hilo.
FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 240
FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 240
OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUMALIZA NUSU MUHULA KIDATO CHA KWANZA
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI 2025
MUDA 2:30
MAELEKEZO
1. Karatasi hii Ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi 10
2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa
3. Sehemu A na C Zina alama kumi na Tano (15) Kila na sehemu B Ina alama sabini (70)
4. Zingatia maelezo ya Kila sehemu na ya Kila swali
5. Andika jina lako juu ya karatasi hii.
SEHEMU A. Alama 15
1. Chagua jibu sahihi kutoka machuguzi uliopewa kwa vipengele (i)- (x) kasha andika jibu lake katika nafasi uliopewa.
i) Somo la historia ya Tanzania na maadili linaundwa na dhana kuu mbili nazo ni
ii) Ni miongozo inayotawala tabia na matendo ya mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla. dhana hii imebebwa na neno
iii) Neno maadili linapotumika huweza pia kuashiria au kuimarisha Tunu za jamii au taifa ni zipi Kati ya zifuatazo
vi) Tunaweza kuwakaribisha wageni kwa furaha na kuwapa heshima kubwa ikiwa pamoja na kukirimiwa kwa
v) Mazingira ya kiliografia yanaweza kuathiri shughuli za binadamu kama vile
vi) Kwa kutumia uchambuzi wa makabila Tanzania ni nchi yenye makundi ya makabila yote yanayopatikana barani Afrika makundi hayo ni
vii) Kihistoria kundi kubwa la tatu la watanzania ambalo ni jamii ya wafugaji walioingia nchini Tanzania wakitokea kusini mwa sudani ni
viii) Jamii za wakushito zinahusisha makabila kama
ix) Kwa hapa Tanzania jamii za Wanilo ni kama
x) Morani ni kundirika katika jamii ya kimasai la vijana wenye umri Kati ya miaka
A) 18 na 35
B)18 na 40
C)18 na 60
D) 18 na 80
2. OANISHA JIBU LA ORODHA 'A' NA JIBU LA ORODHA 'B'
| ORODHA A | ORODHA B |
|
|
SEHEMU B. Alama 70
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Mkude ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya wavulana buingu . Ameshindwa kuelewa maana ya maneno yafuatayo kwenye somo la historia ya Tanzania na maadili. Msaidie kumuelezea maana ya maneno hayo.
a) Tunu za taifa
b) maadili
c) Jiografia
d) Jamii
e) wajibu
4. Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza mkondo A waelezee wanafunzi wenzako umuhimu wa kuwa na maadili katika jamii na taifa kwa ujumla.
5.Warioba ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza alichaguliwa na jamii yake kuelezea namna ambavyo vijana wanaweza kujengwa kwa kuwa na tabia njema. Msaidie warioba katika kuwaeleza vijana vitu vinavyojenga tabia njema katika jamii zetu nukta Tano.
6. Ukiwa Kama mwanafunzi kutoka shule ya sekondari chekeleni. waelezee wanafunzi wenzio kwanini jamii za Asili ya kitanzania zilihama kutoka eneo Moja kwenda eneo jingine nukta Tano
7. Kwa kutumia nukta Tano tofautisha jamii za Asili za wakichembe na jamii za Asili za kibantu.
8. Kwa kumtumia mtaalamu "EMILE DURKHEIM" (1884) Toa dhana ya neno 'Jamii'
9. Eleza Tofauti iliyopo Kati ya maadili yaliyojengwa katika jamii za Asili na jamii za sasa za kitanzania
SEHEMU C Alama 15
Jibu swali la kumi
Bainisha changamoto za kukuza maadili katika jamii unamoishi na Kisha toa mapendekezo ya jinsi ya kuzitatua.
FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 201
FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 201