FORM THREE EDK ANNUAL EXAMS

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA PILI

ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

KIDATO CHA TATU 

MUDA: SAA 2:30 NOVEMBER 2025

Maelekezo:

  1. Mtihani huu Una sehemu A, B na C
  2. Jibu maswali yote kutoka sehemu zote.
  3. Udanganyifu wa Aina yeyote ni haramu.
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
  5. Andika jina lako kamili katika kila ukurasa wa karatasi yako ya majibu. 

SEHEMU A (Alama 16) 

Jibu maswali yote.

1. Katika kipengele i -x chagua jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu lako katika kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A

1.(i) Ni upi mtazamo wa Uislamu juu ya maada ya ‘ibada’?

  1. Ni kufuata amri za Allah zote kwa kuchunga mipaka yake katika maisha ya kila siku
  2. kipengele cha maisha yake ya kila siku kibinafsi na kijamii.
  3. ina maaana ya utumwa
  4. ina maaana ya unyenyekevu 

(ii) Nini maana ya Dini. 

  1. Ni njia ya maisha
  2. Ni mzunguko wa maisha
  3. Ni utaratibu wa wanadamu
  4. Ni mfumo wa maisha ya mwanadamu

(iii) Nini maana ya shirki. 

  1. kulinganish
  2. kufananisha
  3. Shirk ni kinyume cha Upweke au Umoja (Tawhiid)
  4. Ni dhulma kubwa kuliko zote.

(iv) Ni ipi maana halisi ya kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w) katika maisha ya kila siku? 

  1. kusali sana na kufunga.
  2. Ni kufuata amri za Allah zote kwa kuchunga mipaka yake katika maisha ya kila siku. 
  3. kutoa zaka ya mali
  4. kwenda kuhiji kwa mwenye uwezo

(v) Matendo ya ibada ya Hijjah.

  1. Twawafu na kusai
  2. kusai na kusoma Qur an
  3. Twawafu na kusali sunnah
  4. kuzuru makkah

(vi) Bainisha nafasi ya Zakat katika Uislamu. 

  1. Ni amri ya Allah
  2. Ni nguzo ya imani
  3. Ni nguzo ya ihsani
  4. ni nguzo ya swala

(vii) Eleza maana ya swaumu kisheria 

  1. Ni amri ya Allah.
  2. ni nguzo ya imani
  3. kujizuia kula na kunywa
  4. kujizuia na kazi

(viii) Wengi wafungao mwezi wa Ramadhan hawafikii malengo ya funga zao. Sababu ya ni ? 

  1. kuto futuru mapema
  2. kuto Sali tarawehe
  3. kuto kula daku
  4. kuto zingatia masharti ya swala

(ix) Miongoni mwa haki katika Uislamu ni. 

  1. Haki za kitaifa
  2. Haki za Viumbe na Mazingira.
  3. Haki za kustarehe
  4. Haki za kutembea

(x) Hii ni haki kisheria ili kuwa mwanafamilia halali.

  1. haki ya nasaba
  2. Haki ya kuishi
  3. Haki ya kujenga
  4. Haki ya urafiki


i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x











2. Oanisha kifungu cha maneno kilichopo kutoka ORODHA "A" na kile kinachowiana kutoka ORODHA "B" kisha andika herufi ya jibu lako katika kijitabu chako cha kujibia.

ORODHA A

ORODHA B

  1. Malaika mkuu anaye mhusika na kupeleka wahyi
  2. Kumchunga na Kumlinda kila mtu na kuandika amali zake nzuri na mbaya.
  3. Kutoa roho za viumbe.
  4. Kuzihoji, kuzistarehesha au kuziadhibu roho za wafu kaburini.
  5. Kupuliza Parapanda siku ya Qiyama. 
  6. Kuwaliwaza na kuwakaribisha watu wema peponi.
  1. Mikail
  2. Ridhwani
  3. Israfil
  4. Munkar na Nakir
  5. Malakul Mauti
  6. Raqibu na atidi
  7. Jibril


i

ii

iii

iv

v

vi







SEHEMU B

3. Dhihirisha matunda ya kusimamisha ibada ya swala kikamilifu.

4. . Kwa kutumia ushahidi wa Hadith, onesha hatua tatu za kuondosha uovu katika mazingira ya jamii yako.

5. Orodhesha itikadi ya makundi ya dini za wanaadamu zifuatazo; 

  1. Ukafiri 
  2. Ushirikina 
  3. Utawa

6. Kutokana na ushahidi wa kihistoria, eleza uwepo wa ufufuo baada ya kufa.

7. Ni lipi lengo la kuletwa Mitume na Manabii?

8. Ainisha mafunzo matano yatokanayo na mkataba wa Hudaibiyah kwa muhtasari.

 SEHEMU C

9. Eleza hatua alizochukua Mtume (s.a.w) katika kuihifadhi na kuilinda Qur’an.

10. Mwanaadamu pamoja na ujuzi alionao, hawezi kujiundia mfumo sahihi wa maisha. Thibitisha kauli hii kwa hoja tano tu.

11. Mtume (s.a.w) alitumia njia za ulinzi, usalama na diplomasia katika kuilinda serikali ya Kiislamu Madinah. Fafanua kauli hii.

FORM THREE EDK EXAM SERIES 253  

FORM THREE EDK EXAM SERIES 253  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256