Sura ya 01 : Dhana ya ramani

Utangulizi

Mandhari ya uso wa dunia hutofautiana kutoka eneo moja kwenda lingine. Katika halt ya kawaida ni vigumu kufahamu mandhari ya mahali fulani pasipo kutembelea eneo husika. Ramani ni mwongozo unaorahisisha ujifunzaji kuhusu eneo fulani linalopatikana katika uso wa dunia bila kufika katika eneo husika. Katika sura utajifunza maana ya ramani, aina za ramani, vipengele muhimu vya ramani, sifa za ramani, na umuhimu wa ramani. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kufafanua aina za ramani katika miktadha mbalimbali.

Fikiria

Mwonekano wa maeneo mbalimbali ya uso wa dunia

Maana ya ramani

Ramani ni mchoro unaowakilisha taarifa zilizopo katika uso wa dunia kwa kutumia skeli maalumu. Ramani huchorwa katika karatasi, kitambaa, kidijitali au eneo lolote baps. Taarifa za kijiografia zinazoweza kuwasilishwa katika ramani ni kama vile; milima, mabonde, mito, barabara, majengo na taarifa zingine muhimu. Ramani husaidia kuelewa jinsi maeneo yalivyo na namna ya kuyafikia.

Zoezi Ia kwanza

1. Kwa nini tunahitaji ramani?

2. Eleza tofauti iliyopo kati ya picha na ramani.

Aina za ramani Vigezo mbalimbali hutumika kuainisha aina za ramani. Kigezo kimojawapo ni kuangalia lengo Ia ramani husika. Kwa kutumia kigezo hiki, kuna makundi makuu mawili ya ramani. Makundi hayo ni: ramani za jumla na ramani za thematiki.

Ramani za jumla

Hizi ni ramani zinazotoa taarifa za jumla kuhusu eneo fulani. Ramani hizi hazitoi taarifa moja pekee, ball hutoa taarifa mbalimbali za eneo husika. Kwa mfano; barabara, mito, mipaka ya kiutawala, makazi ya watu, milima na uoto. Ramani hizi humsaidia mtumiaji kuelewa taarifa za msingi za mahali fulani, uhusiano wa vitu mbalimbali vilivyopo, pamoja na kutambua uelekeo katika uso wa dunia. Hivyo, ramani za jumla ni kama vile; ramani za topografia, ramani za kisiasa, na ramani za barabara na reli.

Ramani za topografia

Ramani hizi huwakilisha mwonekano wa maumbo mbalimbali ya asili na yaliyotengenezwa na binadamu yanavyoonekana katika uso wa dunia. Pia, hutumia mistari ya kontua kuonesha tofauti za miinuko katika eneo husika la ardhi. Mfano wa maumbo ya asili ni kama vile: bahari, maziwa, mito, tambarare, mabonde, milima, na uoto. Mfano wa maumbo yaliyotengenezwa na binadamu ni pamoja na majengo, na barabara, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 1. Hivyo, ramani hizi ni muhimu katika kupanga shughuli za aina mbalimbali kama vile ujenzi, utalii, kilimo, viwanda, uvuvi na biashara.

Ramani Ya Topografia Mkoa Wa Tanga


Kielelezo namba 1: Topografia ya Mkoa wa Tanga

Ramani za kisiasa Ramani hizi zinatoa taarifa kuhusu mipaka ya nchi, mikoa, wilaya na maeneo mengine ndani ya nchi. Pia, zinaonesha maeneo muhimu kama vile: majengo ya serikali, pamoja na miji mikuu au muhimu, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 2. Ramani za kisiasa ni muhimu kwa watafiti, wanafunzi na wageni wanaohitaji kuelewa mipaka ya kiutawala ya eneo fulani.

Ramani za kisiasa huweza kubadilika baada ya muda fulani. Baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha mabadiliko kwenye ramani za kisiasa ni pamoja na vita, migogoro ya mipaka kati ya nchi na nchi, kuundwa kwa taifa jipya, makubaliano ya kisiasa, na mabadiliko ya mipaka ndani ya nchi. Kwa sababu ya mambo haya, ramani za kisiasa huchorwa upya iii kuonesha muonekano wa sasa wa nchi au eneo husika.

Ramani Ya Tanzania Ya Mipaka Na Tawala Za Mikoa


Kielelezo namba 2: Mipaka ya Tawala za mikoa

Ramani za barabara na reli Ramani hizi zinatoa taarifa muhimu kuhusu mitandao ya barabara na reli, kama vile; barabara kuu, na za Mitaa, na alama muhimu za eneo fulani, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 3. Pia,

zinaonesha umbali kati ya eneo moja na jingine, na mara nyingi hutoa taarifa kuhusu vituo vya mafuta, migahawa na hoteli. Ramani za barabara na reli ni muhimu kwa madereva na wasafiri.

Ramani Ya Mtandao Wa Reli Na Barabara Tanzania


Kielelezo namba 3: Mtandao wa barabara na reli Tanzania

Zoezi la 02

1. Utatumia aina gani ya ramani kukuongoza kwenda mkoa ambao haujawahi kufika?

2. Kwa nini ramani za kisiasa hubadilika baada ya muda?

3. Iwapo unataka kupanda mlima, ni ramani gani utaitumia kufahamu mwinuko wa mlima huo?

Ramani za thematiki

Hizi ni ramani zinazowasilisha mada au taarifa moja maalumu na pekee. Ramani za thematiki zinaweza kuwa za aina mbalimbali kulingana na mada inayowasilishwa. Kwa mfano, ramani za thematiki zinaweza kuwasilisha aina ya udongo, uoto, mazao, idadi ya watu, hali ya hewa na mipango mji.

Ramani ya idadi ya watu

Ramani hii inaonesha wingi au mtawanyiko wa watu katika eneo fulani. Ramani za idadi ya watu zinatusaidia kuona maeneo yenye watu wengi au wachache. Zinasaidia watu wanaopanga kuhusu mahali pa kuweka vitu muhimu kama shule, hospitali, masoko, na barabara. Kielelezo namba 4 kinaonesha ramani ya mtawanyiko wa watu katika mkoa wa Tabora mwaka 2022.

Ramani Ya Mtawanyiko Wa Watu Katika Mkoa Wa Tabora


Kielelezo namba 4: Mtawanyiko wa watu katika Mkoa wa Tabora

Ramani za hali ya hewa Ramani hizi zinaonesha mtawanyiko wa hali ya hewa katika eneo fulani. Zinaonesha vipengele vya hall ya hewa kama vile; joto, mvua, upepo, unyevu-anga, na mgandamizo wa hewa unavyotofautiana kati ya eneo moja na lingine. Ramani hizi ni muhimu kwa shughuli za kilimo, biashara, utalii na usafirishaji. Kielelezo namba 5 kinaonesha mtawanyiko wa mvua katika mkoa wa Iringa.

Ramani Ya Mtawanyiko Wa Watu Katika Mkoa Wa Iringa


Kielelezo namba 5: Mtwanyiko wa mvua Mkoa wa Iringa

Ramani za mipango miji Ramani hizi zinaonesha mpangilio wa miji na vggi kwa ajili ya makazi na huduma za kijamii. Kwa mfano, mpangilio wa nyumba, maduka, shule, hospitali na barabara, kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 6. Ramani hizi hutumiwa zaidi na maafisa ardhi na mipango miji.

Ramani Ya Mipango Miji


Kielelezo namba 6: Ramani ya mipango miji

Zoezi la tatu

1. Kwa nini ramani za thematiki zinaweza kutofautiana sana hata kama zinaonesha eneo moja?

2. Iwapo kuna dharura ya moto katika mtaa wako, ni aina gani ya ramani ungetumia kuwaelekeza wataalamu wa kuzima moto kufika eneo hilo?

3. Chunguza jedwali lifuatalo, kisha pendekeza aina ya ramani inayoweza kutumiwa na watu wafuatao.

Na

Mtu

Aina ya ramani

1

Mjenzi


2

Dereva


3

Mtalii


4

Mkulima


KAZI YA KUFANYA NAMBA 1

Chunguza Kielelezo namba 7, kisha jibu maswali yanayofuata:

Kielelezo namba 7: Aina za ramani

1. Bainisha aina za ramani A, B, C na D kama zilivyowasilishwa kwenye Kielelezo namba 7.

2. Bainisha ramani za thematiki na ramani za jumla katika Kielelezo namba 7.

Vipengele muhimu vya ramani Vipengele muhimu vya ramani ni sehemu za msingi za ramani zinazowezesha matumizi ya ramani husika. Maana na uhalisia wa ramani umebebwa na sehemu hii muhimu. Vipengele hivi hufanya ramani ieleweke na wenye kuwasilisha taarifa za eneo husika kwa usahihi. Vifuatavyo ni vipengele muhimu vinavyotakiwa kuzingatiwa katika ramani:

(a) Fremu: ni mpaka au mstari wa nje unaozunguka ramani. Fremu inasaidia kuweka wazi mipaka ya ramani na kuitenganisha na taarifa nyingine kwenye ukurasa. Inaonesha ramani inapoanzia na inapoishia;

(b) Kichwa cha ramani: Husaidia kuitambulisha ramani kwa msomaji kuwa ramani inahusu nini au inawasilisha taarifa au jambo gani la kijiografia. Kwa mfano, kama ramani inaonesha barabara za Tanzania, kichwa cha ramani kinaweza kuwa "Ramani ya barabara za Tanzania";

(c) Uelekeo wa Kaskazini: Huonesha uelekeo katika ramani ambao kwa kawaida huwasilishwa na alama ya ncha ya Kaskazini. Alama hii inamwezesha msomaji kubaini pande zingine za dunia katika ramani kama vile; Kusini, Mashariki na Magharibi. Kujua uelekeo katika ramani kunakusaidia kuelewa mahali vitu vilipo kwenye ramani;

(d) Ufunguo: Unafafanua ishara na alama zilizotumika katika ramani. Kwa mfano, alama ya mti inaweza kuwakilisha msitu; na mstari wa mawimbi wenye rangi ya bluu unaweza kuwakilisha mto;

(e) Skeli: Inaonesha uhusiano wa umbali uliotumika katika ramani na umbali halisi katika ardhi. Kwa mfano, Sentimeta moja kwenye ramani inaweza kuwakilisha Kilometa kumi katika ardhi;

(f) Mistari ya gridi: ni mistari inayogawanya ramani katika miraba. Mistari hii inakusaidia kupata maeneo mahususi kwenye ramani. Kila mraba una namba au herufi inayokusaidia kupata vitu kwa urahisi;

(g) Chanzo: Kinaelezea mahali palipotumika kupata taarifa zilizowasilishwa kwenye ramani. Chanzo kinaweza kuwa shirika au taasisi ya kiserikali au isiyo ya kiserikali. Kuonesha chanzo cha ramani husaidia kuthibitisha usahihi wake na kuwawezesha watumiaji wengine kuirejelea katika kazi zao. Kielelezo namba 8 kinaonesha vipengele muhimu vya kuzingatia katika ramani.

RAMANI YA TANZANIA


Kielelezo namba 8: Vipengele muhimu vya ramani

KAZI YA KUFANYA NAMBA 2

Chunguza Kielelezo namba 9, kisha jibu maswali yanayofuata


Kielelezo namba 9: Kijiji cha Mwendapole

MASWALI

1. Eleza mapungufu uliyobaini katika Kielelezo namba 9.

2. Bainisha vipengele muhimu vya ramani vilivyopaswa kuwekwa katika herufi A, B, C na D, kisha eleza umuhimu wa kila kipengele ulichobaini.

3. Bainisha aina ya ramani iliyowakilishwa katika kielelezo namba 9.

Sifa za ramani

Ramani nzuri inapaswa kuwa na sifa zifuatazo:

(a) Isomeke na kutafsiriwa kwa urahisi;

(b) ioneshe vipengele vyote muhimu vya ramani, kama vile skeli, fremu, chanzo, ufunguo, mistari ya gridi, kichwa cha ramani na uelekeo wa Kaskazini;

(c) iwakilishe maeneo na umbali halisi, pamoja na kuweka vitu kwa usahihi;

(d) itumie rangi na maandishi yanayoonekana iii kusaidia watumiaji kuelewa vizuri;

(e) ioneshe taarifa pekee zinazohitajika kwa madhumuni husika;

(f) itumie alama, rangi na mitindo inayofanana kwenye ramani yote iii ieleweke kwa urahisi; na

(g) iwe na taarifa za hivi karibuni iii kuhakikisha kila kitu kinachooneshwa ni sahihi.

Umuhimu wa ramani Ramani ni kama kitabu cha mwongozo wa dunia kinachotusaidia kujifunza kwa kuchunguza na kuelewa sehemu zinazotuzunguka. Hivyo, ramani ni zana muhimu sana ambayo hutumiwa na watu katika miktadha mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya sababu muhimu za kutumia ramani.

(a) Kujifunza kuhusu maeneo mbalimbali, hata kama hatujawahi kufika;

(b) kufahamu umbali kutoka sehemu moja hadi nyingine;

(c) kufahamu uelekeo wa kufuata iii kufika tulikokusudia, kama Kaskazini, Kusini, Mashariki, au Magharibi;

(d) kupanga safari zetu kwa kubaini barabara bora, njia za mkato na maeneo ya kuvutia tunayoweza kuyaona njiani;

(e) kuyafahamu mazingira yetu na vitu vilivyomo, kama vile milima, mito, maziwa na misitu;

(f) kusaidia wakati wa dharura, kama vile majanga ya moto na mafuriko kwa kusaidia timu za uokoaji kubaini njia bora za kufika eneo la tukio;

(g) kusaidia kujifunza kuhusu hali ya hewa katika maeneo mbalimbali kwa kuonesha mtawanyiko wa mvua, uoto na shughuli za binadamu zinazofanyika;

(h) kuonesha mahali ambapo rasilimali muhimu za nchi zinapatikana. Kwa mfano, mito, maziwa, misitu na madini;

(i) kuonesha makazi na idadi ya watu katika maeneo tofauti;

(j) kujua mipaka ya kiutawala, kama vile mipaka ya kimataifa, mikoa, wilaya, na

(k) kuonesha vivutio vya utalii kama vile Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na hifadhi za wanyamapori. Hii husaidia kuvutia watalii kutembelea maeneo haya; na

(I) kusaidia kuelewa historia ya mahali kwa kuonesha jinsi palivyobadilika baada ya muda.

Zoezi La nne

1. Eleza jinsi ramani zinavyosaidia kukuza shughuli za utalii.

2. Mkulima anawezaje kutumia ramani?

www.learninghubtz.co.tz

Zoezi la marudio

Sehemu A: Chagua herufi ya jibu sahihi

1. Ramani ni nini?

  1. Uwakilishwaji wa vitu vilivyomo kwenye uso wa dunia kwa kutumia uelekeo wa kaskazini.
  2. Uwakilishwaji wa vitu vilivyomo kwenye uso wa dunia kwa kutumia skeli.
  3. Uwakilishwaji wa vitu vilivyomo kwenye uso wa dunia kwa kutumia ufunguo.
  4. Uwakilishwaji wa vitu vilivyomo kwenye use wa dunia kwa kutumia mistari ya gridi.

2. Aina gani ya ramani huonesha maumbo ya asili na maumbo yaliyotengenezwa na binadamu?

  1. Ramani za topografia.
  2. Ramani za kisiasa.
  3. Ramani za kiuchumi.
  4. Ramani za thematiki.

3. !pi kati ya zifuatazo ni sifa mojawapo ya ramani?

  1. Kuwa na rangi nyingi.
  2. Kuwa na alama nyingi za kuvutia.
  3. Kusomeka na kutafsiriwa kwa urahisi.
  4. Kuwa na maneno mengi ya kisayansi.

4. Ramani zina umuhimu gani katika maisha ya binadamu?

  1. Kupata utaalamu.
  2. Kusaidia kuonesha alama mbalimbali zinazotumika katika ramani.
  3. Kuonesha mahali ambapo rasilimali muhimu za nchi zinapatikana. (
  4. Kuonesha uwezo wa kuchora ramani.

5. Jinsi gani ramani zinaweza kusaidia wakati wa dharura?

  1. Kwa kuonesha jinsi moto unavyowaka.
  2. Kuelekeza namna majanga yanavyotokea.
  3. Kusaidia timu za uokoaji kubaini uelekeo sahihi wa eneo la tukio.
  4. Kusaidia timu za waokoaji kuzima moto.

6. Ramani inawezaje kusaidia kutatua migogoro ya ardhi?

  1. Kwa kuonesha mtawanyiko wa watu.
  2. Kwa kuonesha mipaka ya kiutawala.
  3. Kwa kuonesha uelekeo wa mahali.
  4. Kwa kuonesha umbali kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

7. Ni jinsi gani ramani zinaweza kuwa chanzo cha mapato ya serikali?

  1. Kutoa mwongozo wa maeneo ya vivutio kwa watalii.
  2. Kuonesha maeneo yenye barabara za kisasa.
  3. Kusaidia watu kupata huduma za afya.
  4. Kuonesha maeneo ya sherehe na burudani.

Sehemu B:

8. Oanisha maneno yaliyopo safu A na yale ya safu B kupata maana kamili.

Na.

Safu A

Safu B

. '

Ramani ya topografia

(a) juu ya karatasi, ardhi, kitambaa na kompyuta

ii.

Fremu

(b) huwakilisha maumbo ya use wa dunia

iii. .

Vipengele muhimu katika ramani

(c) uhusiano wa umbali uliowasilishwa katika ramani na umbali halisi uliopo katika ardhi

iv.

Skeli

(d) skeli, fremu, uelekeo wa Kaskazini, kichwa cha ramani, ufunguo, chanzo na mistari ya gridi

v.

Sehemu ambapo ramani inaweza kuchorwa

(e) kuonesha mpaka wa ramani husika



(f) isomeke kwa urahisi kwa watumiaji wa ramani husika



(g) hufafanua alama na ishara zilizotumika katika ramani

C: Maswali ya majibu mafupi:

9. Ramani inapaswa kuwa na sifa zipi? Zitaje kwa kutoa mifano.

10. Ni kwa namna gani ramani za topografia zinatofautiana na ramani za mipango miji?


Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256