?>
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MWISHO WA MWAKA 2026 – DARASA LA TANO
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Jina la Mwanafunzi: __________________________________
Shule: ______________________________
Muda: Saa 1:30 Jumla: Alama 50
MAELEKEZO
SEHEMU A (Alama 20)
1. Chagua jibu sahihi katika kila kipengele kisha andika herufi yake kwenye mabano.
i. Ni taifa gani lililotawala Tanganyika baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia? ( )
ii. Mkataba wa Heligoland uliotiwa saini mwaka 1890 ulihusisha mataifa gani? ( )
iii. Ni kiongozi gani wa Wahehe aliyepinga uvamizi wa Wajerumani? ( )
iv. Vita vya Maji Maji vilipiganwa kati ya miaka ipi? ( )
v. Ni chama gani kilichoanzishwa mwaka 1954 kupigania uhuru wa Tanganyika? ( )
vi. Ni ipi ilikuwa mojawapo ya athari hasi za elimu ya kikoloni? ( )
vii. Ni njia ipi iliyotumiwa na wakoloni kuimarisha utawala wao? ( )
viii. Ni jambo gani lililoathiri mfumo wa jadi wa umiliki wa ardhi wakati wa ukoloni? ( )
ix. Ni tendo lipi linaloonesha kuheshimu maadili ya Kitanzania? ( )
x. Ni kipi kinachosaidia kujenga umoja wa kitaifa na uzalendo? ( )
2. Oanisha matukio katika Orodha A na miaka katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi.
| Orodha A | Jibu | Orodha B |
|---|---|---|
| (i) Kusainiwa kwa Mkataba wa Heligoland | ( ) | A. 1964 |
| (ii) Kuanza kwa Vita vya Maji Maji | ( ) | B. 1954 |
| (iii) Kuanzishwa kwa TANU | ( ) | C. 1920 |
| (iv) Tanganyika kupata uhuru | ( ) | D. 1890 |
| (v) Muungano wa Tanganyika na Zanzibar | ( ) | E. 1961 |
| F. 1905 | ||
| G. 1999 |
3. Jaza nafasi kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye mabano.
Mfumo wa nchi moja kuitawala nchi nyingine kisiasa na kiuchumi huitwa ____________________ (ukoloni / ujamaa).
Kiongozi aliyekuwa akisimamia vibarua mashambani wakati wa ukoloni aliitwa ____________________ (mnyapara / gavana).
Chama kilichotangulia TANU kiliitwa ____________________ (TAA / CCM).
Tabia ya kupenda nchi na kuitumikia kwa uaminifu huitwa ____________________ (uzalendo / ubaguzi).
Kutunza na kuheshimu desturi nzuri za jamii ni njia ya kulinda ____________________ (maadili / ukoloni).
SEHEMU B (Alama 20)
4. Panga matukio yafuatayo kwa mpangilio wa wakati, kuanzia la kwanza hadi la mwisho. Andika herufi A–E katika nafasi sahihi.
A. Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961.
B. Kuanzishwa kwa TANU mwaka 1954.
C. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
D. Kusainiwa kwa Mkataba wa Heligoland mwaka 1890.
E. Vita vya Maji Maji kuanza mwaka 1905.
| Nafasi | Ya kwanza | Ya pili | Ya tatu | Ya nne | Ya tano |
|---|---|---|---|---|---|
| Herufi |
5. Chunguza picha ya Bendera ya Taifa la Tanzania kisha jibu maswali yanayofuata.
![]() |
Alama ya Taifa inayoonekana kwenye picha inaitwaje? ________________________________________________________________
Taja rangi mbili zinazopatikana kwenye bendera hiyo. ________________________________________________________________
Rangi ya kijani katika bendera ya Tanzania huwakilisha nini? ________________________________________________________________
Taja tukio moja la kitaifa ambalo bendera hupeperushwa.________________________________________________________________
Eleza njia moja ya kuonesha heshima kwa Bendera ya Taifa. ________________________________________________________________
SEHEMU C (Alama 10)
6. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Maadili ya Kitanzania yanajengwa kwa kuheshimiana, kushirikiana, kutunza urithi wa jamii na kupenda nchi. Kabla ya ukoloni, jamii nyingi za Kitanzania zilikuwa na mifumo ya uongozi wa jadi, desturi na taratibu za kusaidiana. Wakati wa ukoloni, baadhi ya mifumo hiyo ilibadilika. Elimu na dini za kigeni zilileta mabadiliko katika maisha ya jamii, huku baadhi ya lugha na mila za asili zikidhoofika. Hata hivyo, matumizi ya Kiswahili yalisaidia kuimarisha mawasiliano na umoja miongoni mwa Watanzania.
Baada ya kupata uhuru, Watanzania waliendelea kujenga umoja wa kitaifa kwa kuthamini lugha ya Kiswahili, kuheshimu alama za Taifa na kushiriki shughuli za maendeleo. Kila mwananchi ana wajibu wa kulinda mali ya umma, kuheshimu wengine na kupinga vitendo vya rushwa. Vijana wanaweza kuonesha uzalendo kwa kujifunza historia ya nchi yao, kutunza mazingira na kushirikiana na watu wa jamii mbalimbali.
Taja mfumo mmoja wa jamii uliokuwepo kabla ya ukoloni.________________________________________________________________
Taja mabadiliko mawili yaliyoletwa na ukoloni katika maisha ya jamii za Kitanzania. ________________________________________________________________
Ni lugha gani iliyosaidia kuimarisha mawasiliano na umoja wa Watanzania? ________________________________________________________________
Taja wajibu mmoja wa mwananchi unaotajwa katika kifungu.________________________________________________________________
Eleza njia moja ambayo vijana wanaweza kuonesha uzalendo.________________________________________________________________
MWISHO WA MTIHANI
LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD FIVE EXAM SERIES 158
Jina La Mwanafunzi: _____________________________________
Jina La Shule:_____________________________________
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA WAZIRI MKUU -TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA MUHULA WA KWANZA DARASA LA TANO
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI
Muda: saa 1:30 MEI 2026
SEHEMU A (Alama 20)
i. Kupendana huleta amani na kuwajali watu wengine pia,Ni kitendo gani kati ya vifuatavyo sio sahihi kuwatendea wenzetu?
A. kuwasaidia B. Kushauriana nao C. Kuaminiana D. kuwadhulumu E. kushirikiana ( )
ii. Hapo kale Nchi nyingi za kiafrika zilitawaliwa na mataifa ya kigeni,Je, Hali ya nchi moja kuitawala nchi nyingine kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni inaitwaje?
A. Ubepari B. Ujamaa C. ukoloni D. uzalendo E. utumwa ( )
iii. Viwanda vingi wakati wa ukoloni vilianzishwa hasa kwa ajili ya kuchakata nini?
A. Mazao B. Mkonge C. Tumbaku D. Madini E. Malighafi ( )
iv. Ipi kati ya zifuatazo sio sekta ya uchumi wakati wa ukoloni wa waingereza?
A. kilimo B. viwanda C. madini D. biashara E. afya ( )
v. Kiongozi aliyeongoza jamii ya wahehe kupambana na uvamizi wa wajerumani alikuwa nani?
A. Mkwawa B. Machemba C. Mangi Sina D. Abushiri E. Isike ( )
vi. Mtu aliyepewa dhamana ya kusimamia vibarua wakifanya kazi katika mashamba ya wakoloni alijulikana kama nani? A.Akida B.Jumbe C.Mnyapara D.Liwali E.Gavana ( )
vii. Sayansi na teknolojia ya asili ya kutengenezea moto iligundulika katika kipindi kipi cha zama za mawe?
A. zama za mawe za kati B. zama za mawe za kale C. zama za mawe za mwisho D. zama za chuma E.Zama za mawe za chuma ( )
viii.Ni ngazi ipi katika uongozi wa shule huongozwa na wazazi ambao huchaguliwa na wazazi wenye watoto katika shule husika?
A. Kamati ya shule B. Mwalimu wa Taaluma C. mwalimu wa nidhamu D. Mwalimu mkuu E. kiranja mkuu ( )
ix. Urithi wa historia inayohusu michoro ya mapangoni unapatikana sehemu gani kati ya hizi zifuatazo?
A. Isimila Iringa B. Kondoa Irangi C. Bonde la Ngorongoro D. Olduvai Arusha E.Laetoli Arusha ( )
x. Mwanamama mahiri na shupavu aliyejulikana kama Litti Kidanka ambaye alionesha upinzani mkubwa dhidi ya Wajerumani alikuwa wa kabila gani kati ya haya yafuatayo?
A. Wagogo B. Wanyeramba C. Wangoni D. Wanyaturu E. Wamasai ( )
2. Oanisha mwaka kutoka orodha A na tukio husika kutoka orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano.
| Orodha A | Majibu | Orodha B |
| i. 1890 | | A. Vita vya Maji Maji B. Kuteuliwa kwa Donald Cameroon C. Kusainiwa kwa mkataba wa Heligoland D. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar E. Jina Tanganyika lilizaliwa F. Kifo cha Abeid Amani Karume G. Kifo cha baba wa taifa Mwl. J. K Nyerere |
| ii. 1964 | | |
| iii. 1905 - 1907 | | |
| iv. 1999 | | |
| v. 1920 | |
3. Jaza nafasi zilizoachwa wazi kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye mabano uliyopewa.
i. Mambo ya lazima ambayo mtu hupaswa kuyatenda ili kukabiliana na mazingira yanayomzunguka huitwaje …………………………………...… (haki/wajibu)
ii. Mwaka 1954 chama cha TAA kiliitisha mkutano mkuu kujadili katiba na muundo wake, ambapo katika mkutano huo kulizaliwa chama kipya cha siasa kilichojulikana kama.....................(CCM/TANU)
iii. ………………………………........................ ni miongoni mwa athari chanya za mfumo wa elimu ya kikoloni. (Kuua lugha za asili/Kueneza lugha ya Kiswahili)
iv. Sheria na kanuni zinazoainisha jinsi nchi itakavyoendeshwa huitwa
…………………………………………. (katiba/kitabu)
v. Ujio wa ..................................ulichochea mabadiliko makubwa katika maadili ambayo ni dini ya Kiislam na biashara ya utumwa. (Wajerumani/Waarabu)
SEHEMU B (Alama 20)
4. Umepewa ngazi 4 za uongozi katika serikali ya Wajerumani ambazo hazipo katika mpangilio sahihi. Zipange ngazi hizo kuanzia ngazi ya juu Kwenda chini kwa kuandika herufi ya jibu sahihi.
| Mpangilio usio sahihi | Mpangilio sahihi |
| A. Gavana | i. |
| B. Waziri wa makoloni | ii. |
| C. Baraza la kumshauri Gavana | iii. |
| D. Liwali | iv. |
| E. Afisa Wilaya | v. |
5. Chunguza picha ifuatayo kisha jibu maswali yanayofuata.
Maswali
i. Mnyama huyo hutumika kama alama ya Taifa, je, anaitwaje?
_____________________________________
ii. Alama hiyo ya Taifa ni kiashiria cha uwepo wa nini nchini Tanzania?
_____________________________________
iii. Taja chombo cha usafiri kinachomilikiwa na serikali ya Tanzania ambacho picha ya mnyama huyo huwekwa kama Ishara ya kuonesha kuwa ni mali ya Tanzania
_____________________________________
iv. Mnyama huyu hutumika kama alama ya mficho kwenye
_____________________________________
v. Taja alama za Taifa nyingine mbili (2) unazozifahamu
A)_____________________________________
B)_____________________________________
SEHEMU C (Alama 10)
6.Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata.
Uzalendo ni hali ya mtu kuwa na moyo wa kuipenda na hata kuwa tayari kuifia nchi yake.Uzalendo unajumuisha kuipenda nchi yako kwa kuithamini na kuilinda.Wanamichezo huonesha uzalendo wao pale wanapoipeperusha Bendera ya Taifa lao katika mataifa mengine sambamba na kuimba wimbo wa Taifa lao.Uzalendo hauigizwi bali ni hisia kali za mapenzi kwa nchi kutoka ndani ya moyo mwa raia mwaminifu na mtiifu. Uzalendo upo kwa kila mwananchi anayejitambua na kujithamini pia. Hata hivyo kila mmoja wetu katika nafasi yake anapaswa kuwa mzalendo. Serikali huhimiza viongozi na wananchi kuwa wazalendo na kuzingatia maslahi ya Taifa badala ya maslahi binafsi na kwa kufanya hivyo itapunguza tamaa ya kujilimbikizia mali. Kwa maana hiyo mwananchi anayeipenda Tanzania kwa dhati ya moyo wake, hataweza kushiriki vitendo vya rushwa kamwe.
Maswali
i. Hali ya mtu kuwa na moyo wa kuipenda na hata kuwa tayari kuifia nchi yake huitwa
_____________________________________
ii. Taja viashiria viwili vinavyotumiwa na wanamichezo kuonesha uzalendo kwa nchi yao wawapo katika mataifa mengine
(a)_____________________________________
(b) _____________________________________
iii. Uzalendo haugizwi, je unatoka kwenye moyo wa raia mwenye sifa gani?
_____________________________________
iv. Serikali inahimiza uzalendo na kuzingatia maslahi ya Taifa ili kukwepa nini?
_____________________________________
v. Kuipenda nchi yako kwa moyo wako kunakuepusha na vitendo gani?
_____________________________________
LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD FIVE EXAM SERIES 140
OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MITIHANI WA UPIMAJI NUSU MUHULA - MACHI 2026
HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI DARASA LA V
MUDA: SAA 1:30
Maelekezo
SEHEMU A (Alama 20)
Jibu masuala yote katika sehemu hii.
1. Kwa kila moja ya vipengee (i) - (x), chagua jibu sahihi kutoka kwa chaguzi zilizotolewa na uandike herufi yake katika kisanduku kilichotolewa.
(i) Ukoloni ni nini?
(ii) Mfumo wa mahakama wakati wa ukoloni ulikuwa unategemea nini?
(iii) Katika mfumo wa ulinzi wakati wa ukoloni, wakoloni walitumia nini?
(iv) Athari moja ya mifumo ya kikoloni katika maadili ya Kitanzania ni nini?
(v) Ukoloni uliathiri vipi mifumo ya mamlaka za kijadi?
(vi) Kabla ya ukoloni, maadili ya Kitanzania yalikuwa yanategemea nini?
(vii) Wakati wa ukoloni, mfumo wa elimu ulikuwa unafundisha nini hasa?
(viii) Athari ya ukoloni katika urithi wa Kitanzania ni nini?
(ix) Mfumo wa uongozi wakati wa ukoloni ulikuwa unategemea nini?
(x) Mabadiliko ya maadili wakati wa ukoloni yalikuwa yanahusiana na nini?
2. Linganisha sehemu za mifumo ya ukoloni katika Orodha A na majukumu yake katika Orodha B kwa kuandika herufi ya jibu sahihi karibu na namba ya kipengee katika jedwali lililotolewa.
| Orodha A | Majibu | Orodha B |
| (i) Mahakama wakati wa ukoloni | [ ] |
|
| (ii) Ulinzi wakati wa ukoloni | [ ] | |
| (iii) Uongozi wakati wa ukoloni | [ ] | |
| (iv) Afya wakati wa ukoloni | [ ] | |
| (v) Elimu wakati wa ukoloni | [ ] |
SEHEMU B (Alama 20)
Jibu masuala yote katika sehemu hii.
3. Jaza mapengo kwa maneno sahihi kutoka katika kisanduku kilichotolewa.
Kisanduku: mahakama, ukoloni, maadili, mamlaka za kijadi, urithi, elimu ya kigeni, ulinzi wa wakoloni, mabadiliko, mwendelezo, athari
(i) Kutawaliwa na nchi za kigeni na kutumia mifumo yao ni ________.
(ii) Mifumo ya kiutawala wakati wa ukoloni ilijumuisha ________ na polisi wa kigeni.
(iii) Athari za ukoloni katika maadili ya Kitanzania ni kupotea kwa baadhi ya ________ wa kiutamaduni.
(iv) Ukoloni uliharibu ________ katika jamii za Kitanzania.
(v) Kabla na wakati wa ukoloni, baadhi ya maadili ya Kitanzania yalikuwa na ________ na mabadiliko.
4. Andika SAHIHI kama kauli ni sahihi au SI SAHIHI kama si sahihi.
(i) Mifumo ya kikoloni ilileta sheria za kigeni na kuathiri maadili ya kijadi.
(ii) Ukoloni uliimarisha mamlaka za watawala wa kijadi katika jamii.
(iii) Elimu wakati wa ukoloni ilifundisha maadili ya wakoloni pekee.
(iv) Athari za ukoloni hazikuathiri urithi wa Kitanzania.
(v) Kabla ya ukoloni, maadili ya Kitanzania yalitegemea urithi wa kijadi.
5. Eleza kwa ufupi maneno yafuatayo:
(i) Ukoloni
(ii) Mifumo ya kiutawala wakati wa ukoloni
(iii) Athari za mifumo ya kikoloni katika maadili
(iv) Mabadiliko na mwendelezo wa maadili ya Kitanzania
6. Orodhesha mambo mawili yaliyoathiri mifumo ya kijamii wakati wa ukoloni na mawili katika athari za ukoloni katika jamii.
Mifumo ya kijamii wakati wa ukoloni:
Athari za ukoloni katika jamii:
SEHEMU C (Alama 10)
Jibu masuala yote katika sehemu hii.
7. Eleza umuhimu wa kuelewa historia ya ukoloni katika maadili ya Kitanzania. Toa hoja mbili.
8. Eleza matumizi mawili ya kufahamu athari za ukoloni katika jamii ya kisasa.
LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD FIVE EXAM SERIES 136