?> HISTORIA STANDARD FOUR EXAMS SERIES
HISTORIA STANDARD FOUR EXAMS SERIES

Jina la Mwanafunzi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

Shule . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS UTAWALA WA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA 

MKOA WA DODOMA 

MTIHANI WA MUHULA DARASA LA NNE

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI [06E]

MUDA : Saa 1:30

MAELEKEZO:

  1. Mtihani huu una maswali sita (6) yenye sehemu A na B
  2. Jibu maswali yote kwenye sehemu zote
  3. Andika majibu yote katika nafasi ulizopewa
  4. Majibu yote lazima yaandikwe kwa kutumia kalamu ya wino mweusi au bluu.
  5. Simu za mkononi au nyenzo yoyote hairuhusiwi katika chumba cha mtihani.
  6. Andika jina na namba ya mtihani katika kila ukurasa wa mtihani huu.
KWA MATUMIZI YA WATAHINI TU
Namba ya Swali Alama Sahihi ya Mtahini Sahihi ya Mhakiki
1.


2.


3.


4.


5.


6.


JUMLA


SEHEMU A: (ALAMA 26)

1. Chagua herufi ya jibu sahihi kisha ujaze kwenye kisanduku ulichopewa

i. Kitendo cha kutoa au kupokea kitu chochote kwa lengo la kupewa upendeleo katika jambo fulani au kupata huduma fulani huitwaje? [      ]

A. Zawadi C. Nidhamu B. Rushwa D. Msaada

ii. Tanzania ni nchi iliyoundwa na mataifa mawili; Tanganyika na Zanzibar. Ni lini muungano wan chi hizo ulifanyika?

A. 9/12/1961 C. 14/10/1999 B. 26/12/1964 D. 26/4/1964

iii. Ipi miongoni mwa tabia zifuatazo huonyesha kitendo cha heshima?

  1. Kumpisha mkubwa kukalia kiti kwenye gari 
  2. Kukataa kuagizwa na mkubwa wako 
  3. Kucheza na wanyama
  4. Kutumia lugha mbaya

iv. Katika historia ya Tanzania, Ni mreno gani wa kwanza kuingia pwani ya Afrika Mashariki?

  1. Mwl. J.K. Nyerere 
  2. Dr. Louis Leakey 
  3. Vasco da Gama
  4. Sultan Seyyid Said

v. Kitu chochote ambacho mtu anastahili kupewa huitwaje?

A. Haki C. Mali B. Wajibu D. Majukumu

2. Oanisha maelezo yaliyopo kwenye orodha A na majibu yaliyopo kwenye orodha B, na kisha uandike herufi ya jibu sahihi kwenye chumba ulichopewa.

ORODHA A MAJIBU ORODHA B
(i) Majengo ya zamani yaliyobaki kama sehemu ya historia na utamaduni.
  1. Makavanzi
  2. Makumbusho
  3. Masimulizi
  4. Maeneo ya kiakiolojia
  5. Magofu

(ii) Sehemu ambapo nyaraka na taarifa mbalimbali za kihistoria huhifadhiwa.
(iii) Maeneo yanapopatikana masalia ya mambo ya kale na utamaduni wa mwanadamu.
(iv) Maeneo yanayotumiwa kuhifadhi vitu vyenye historia na urithi wa kiasili na kiutamaduni.

3. Chagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku kasha jibu maswali yanayofuata;

Kaole, Zanzibar, Olduvai Gerge, Zinjanthropus, Link

(i) Mji palipogundulika mabaki ya Dinosaria wa Tendaguru.

image

(ii) Sehemu ambapo lipo jengo la maajabu ambalo lina historia ya kuwa jengo la kwanza kuwekwa lifti za umeme.

image

(iii) Eneo lilipogunduliwa fuvu la Binadamu wa kale na Dr. Louis Leakey.

image

(iv) Jina lilopewa fuvu la binadamu wa kale lililogunduliwa mwaka 1959.

image

(v) Mji yanapopatikana magofu ya msikiti na kituo cha kuhifadhia watumwa.

image

SEHEMU B: (ALAMA 24)

4.  Ainisha matendo yafuatayo kwa kusoma maelezo yake na kuweka alama ya vema (√) katika chumba sahihi. Kipengele cha tano (v) kimefanywa kama mfano kwa ajili yako.

Kitendo

Kitendo cha kimaadili

Kitendo kisicho cha kimaadili

(i) Kupigana na wenzako



(ii) Kusalimia watu wakubwa



(iii) Kushirikiana na watu wengine



(iv) Kuwatukana watu wazima



(v) Kumsaidia mzee kubeba mizigo


5.  Tazama picha hizi kwa makini kasha jibu maswali yanayofuata

Maswali

i. Mwanamke aliyeoneshwa katika picha A anafanya nini?

image

ii. Mwanaume anayeonekana kwenye picha B anafanya nini?

image

iii. Jamii ya mtu aliyeoneshwa kwenye picha B hupendelea kula chakula gani.

image

iv. Aina ya nguo aliyoivaa mtu aliyeoneshwa kwenye picha B inaitwaje?

image

6. Soma habari ifuatayo kasha ujibu maswali yanayofuata;

Jamii za Tanzania hapo Kale zilifanya biashara na wafanyabiashara kutoka Mashariki ya Mbali na ya Kati. Nchi hizo ni India, Irani, Iraki, Kuwait, China na Saud Arabia. Biashara hii ilifanyika katika miji iliyopo katika mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi kama vile Dar es Salaam, Bagamoyo, Tanga, Kilwa na Zanzibar. Biashara hizi zilifanyika kwa kubadilishana bidhaa. Bidhaa kubwa katika biashara hii kutoka nchini ilikuwa dhahabu na pembe za ndovu. Dhahabu ilitoka Zimbabwe kupitia bandari ya Sofala, Msumbiji. Kutoka kwa wageni kuja nchini, bidhaa kubwa zilikuwa shanga na vyombo vya ndani kama vile mabakuli na sahani za udongo. Baadhi ya mabaki ya bidhaa hizi yapo katika Makumbusho hapa nchini, kama vile makumbusho ndogo iliyopo Kaole, Bagamoyo.

Maswali

(i) Mabaki ya bidhaa zilizotumika katika biashara na watu wa Mashariki ya mbali zimehifadhiwa wapi?

image

(ii) Taja bidhaa mbili zilizokuwa zinaletwa kutoka kwa wageni?

image

(iii) Tja nchi mbili za Mashariki ya mbali zilizotajwa kwenye habari hii?

image

(iv) Taja miji miwili iliyopo katika Mwambao wa Pwani

image


LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD FOUR EXAM SERIES 114

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

JARIBIO LA NUSU MUHULA-MACHI 2025 DARASA LA NNE

SOMO: HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

DARASA LA NNE

SEHEMU A: CHAGUA HERUFI YA JIBU SAHIHI

1. Chagua herufi ya jibu sahihi kisha iandike kisanduku cha kujibia 

i. Zifuatazo ni haki za mtoto isipokuwa  

(A) kupata elimu bora 

(B) kutomsikiliza anapohitaji msaada 

(C) kupata nafasi ya kucheza 

ii. Kwa majibu wa sheria ya mtoto ni mtu mwenye umri wa miaka rningapi? 

(A) chini ya miaka 10 

(B) chini ya miaka 18 

(C) chini ya miaka 21 

(D) chini ya miaka 15 

iii. Mfumo wa uongozi wa usultani ulitumika katika maneno gani? 

(A) visiwa vya zanzibari

 (B) kaskazini mwa Tanzania 

(C) kusini magharibi mwa Tanzania 

(D) maeneo ya ziwa Tanganyika  

iv. Familia ya mzee lazier na ile ya mzee moleli zina uhusiano wa damu, kipi ni ukweli kuhusu familia.hizi? 

(A) asili yake ni ukoo mmoja 

(B) zinapatikana kutoka jamu ya kisultani 

(C) kiongozi wake ni mtemi 

(D) zinatokana na makabila tofauti 

 

v. Mtemi alikwa na majukumu yafuatayo isipokuwa  

(A) kusimamia ibada za jamii 

(B) kutengeneza zana za chuma 

(C) kuhusisha migogoro katika jamii 

(D) kusimamia biashara katika himaya yake  

2. Oanisha kufungu cha maneno ya kifungu A dhidi ya kifungu cha maneno ya sehemu B kisha uandike herufi ya jibu sahihi katika mabano.

KIFUNGU A

KIFUNGU B

i. Wahehe 

ii. Wamasai 

iii. Wanyamwezi 

iv. Wahaya 

v. Wachaga

A. Mtemi 

B. Mtwa 

C. Mangi 

D. Omukama 

E. laiboni 

 3. Jaza nafasi zilizo wazi kwa kuchagua jibu sahihi kutoka kwenye kisanduku cha majibu. 

Akiologia

Kusimulia

2009

2019

Usultani

Ustawi wa jamii

Ukoo

Kitemi

 i. Kundi la watu wenye nasaba moja, wakijumlisha familia zenye uhusiano wa damu huitwaje?  

ii. Mfumo wa uongozi wa jadi ulioshamiri zaidi katika visiwa vya unguja na pemba uliitwaje  ........................................................

iii. Sheria ya mtoto ilitungwa mwaka  ........................................................

iv. Mtoto ambaye Haki zake zimekiukwa anaweza kwenda kutoa taarifa kwenye ofisi ya  ........................................................ 

v. Je, ni nini maana ya kuelezea jambo au habari kulingana na mlolongo wa matukio?  

SEHEMU B: MAJIBU MAFUPI

4. Kamilisha jedwali lifuatalo kwa kuandika mkoa ambao eneo Ia kihistoria linapatikana. 

Eneo la kihistoria

Eneo na mkoa ilipo

i. Magofu_ya husuni kubwa

 

ii. Gofu la ngome ya gereza

 

iii. Jumba la caravan serai 

 

iv. Gofu la msitiki mkuu

 

 5. Chunguza picha kisha jibu maswali yanayofuata 

(a) Watu wanaonekana katika picha wametoka kufanya shughuli gani? 

(b) Jaza zana mbili za chuma waliotumia watu wa jamii hii kufanyja shughuli hizo 

(i) ........................................................

(ii) ........................................................

(iii) ........................................................

(c) Taja malighafi iliyotumika kutengeneza nguo walizovaa watu wanaonekana katika picha ........................................................ 

(d) Unafikiri hawa ni wa kabila gani hapa Tanzania? 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD FOUR EXAM SERIES 113

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256