?> JIOGRAFIA STANDARD THREE EXAMS SERIES
JIOGRAFIA STANDARD THREE EXAMS SERIES

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MTAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA AGOSTI 2025

MTIHANI WA  DARASA LA III 

JIOGRAFIA NA MAZINGIRA

Andika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano

(i). Ni somo lipi linalohusu dunia, angahewa, na vitu vilivyopo juu ya uso wa dunia na mtawanyiko wake? 

  1. Hisabati 
  2. Kiswahili 
  3. Jiografia 
  4. Sayansi [    ]

(ii). Ili mazingira yapendeze tunapaswa kufanya nini?

  1. kukata miti 
  2. kuyachafua 
  3. kuyahama 
  4. kuyasafisha na kuyatunza [    ]

(iii). Mazao na mimea hustawi vizuri katika kipindi kipi? 

  1. Kipindi cha jua kali
  2. Kipindi cha usiku 
  3. Kipindi cha baridi 
  4. Kipindi cha mvua [    ]

(iv). Ni vitu gani huonekana angani wakati wa usiku?

  1. nyota na mwezi 
  2. jua na nyota 
  3. mimea 
  4. mvua [    ]

(v). Ni kitu kipi kati ya vitu vifuatavyo huunda mazingira ya kutengenezwa na binadamu? 

  1. milima 
  2. hewa 
  3. mito 
  4. majengo [    ]

(vi). Tabianchi ya sehemu moja hutofautiana na ya sehemu nyingine kwa sababu zipi?

  1. watu waliopo 
  2. sura ya nchi na uoto uliopo 
  3. Wanyama wakali 
  4. Jua [    ]

(vii). Ufugaji wa nyuki hutegemea uwepo wa rasilimali gani muhimu? 

  1. Maji, majani na miamba 
  2. Miti, maua na misitu 
  3. Milima na mabonde 
  4. Mvua na udongo [   ]

(viii). Maeneo ya Tanzania yaliyopo karibu na bahari mara nyingi huwa na hali ya hewa gani? 

  1. Baridi kali 
  2. Baridi na joto 
  3. Joto 
  4. Unyevunyevu [   ] 

2. Oanisha fungu A na B ili kupata maana kamili

Fungu A

Fungu B

(i). Kupanda miti [    ]

(ii)Mazingira  [    ]

(iii). kufagia  [    ]

(iv) Kupanda viunga vya maua [    ]

(v). Madarasa, madawati na bendera ya taifa [   ]

(vi). Mazingira ya nyumbani [    ]

  1. Kitendo cha kusafisha mazingira
  2. Vitu vyote vinavyotuzunguka
  3. Mazingira ya shuleni
  4. Huboresha na kupendezesha mazingira
  5. Kutunza mazingira
  6. Kabati la nguo, mifugo na vyumba vya kulala

 3. Soma habari kisha jibu maswali 

Mazingira ni jumla ya vitu vyote vinavyotuzunguka. Mazingira yamegawanyika katika sehemu mbili ambayo ni mazingira ya asili na mazingira ya kutengenezwa na binadamu. Mazingira ya asili yanajumuisha vitu kama hewa, milima, mito na uoto wa asili. Mazingira ya kutengenezwa yanaundwa na vitu kama majengo, samani na rasilimali nyinginezo.

Ili mazingira yapendeze tunapaswa kuyasafisha na kuyaboresha kwa kupanda miti.

MASWALI

(i). Vitu vyote ninavyomzunguka binadamu vinaunda nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(ii). Milima, mito na hewa ni aina ipi ya mazingira? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(iii). Taja kitendo kimoja tu cha kusafisha mazingira. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(iv). Tunaweza kuboresha mazingira ya shuleni na nyumbani kwa kufanya nini? . . . . . . . . . . . .

(v). Ili mazingira yapendeze yatupasa kufanya nini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

(vi). Taja aina mbili za mazingira. i. . . . . . . . . . . . . . . . . . ... 

ii. . . . . . . . . . . . . . . . ..

(vii). Taja vitu viwili tu vinavyounda mazingira uliyopo

(a). . . . . . . . . . . . . 

(b). . . . . . . . . . ...

4. Chunguza picha ifuatayo kisha jibu maswali

image

 MASWALI

(i). Picha hiyo inaonesha mazingira ya wapi? . . . . . . . . ..

(ii). Taja vitu viwili tu unavyoviona kwenye picha hiyo.

(a). . . . . . . . . . . . . . . . . . ... (b). . . . . . . . . . . . . . ...

(iii). Taja rasilimali mbili tu zinazoweza kupatikana ndani ya majengo hayo. 

(a) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(b) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(iv). Ni huduma gani inayotolewa katika mazingira hayo? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

LEARNINGHUBTZ.CO.TZJIOGRAFIA STANDARD THREE EXAM SERIES 103

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256