?> HISTORIA STANDARD THREE EXAMS SERIES
HISTORIA STANDARD THREE EXAMS SERIES

OFISI YA RAIS-TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MTAA

MTIHANI WA NUSU MUHULA AGOSTI 2025

MTIHANI WA  DARASA LA III 

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

1. Andika herufi ya jibu sahihi kwenye mabano

(i). Elimu inayohusu matukio yaliyotokea nchini Tanzania tangu mwanzo wa maisha ya watu mpaka leo inaitwaje? 

  1. maadili 
  2. Historia ya Tanzania 
  3. Fizikia 
  4. mazingira [   ]

(ii). Kipi kati ya vitendo vifuatavyo ni kitendo cha maadili mema? 

  1. kuiba vipande vya nyama nyumbani
  2. kudanganya
  3. kutukana
  4. kuwapokea wakubwa mizigo [   ]

(iii). Mfululizo wa mambo yaliyotokea katika maisha yetu katika vipindi tofauti huitwaje?

  1. historia 
  2. mazingira 
  3. maadili 
  4. uadilifu [   ]

(iv). Hayati John Pombe Magufuli alifariki tarehe 17 mwezi Machi 2021. Je, katika Maisha yetu hili ni tukio gani? 

  1. la kimaadili 
  2. la kihistoria 
  3. la kufurahisha 
  4. lisilofaa [   ]

(v). Ipi ni faida mojawapo ya vitendo vya kimaadili? 

  1. hujenga tabia ya kuheshimiana
  2. husababisha kubaguana 
  3. huleta ugomvi 
  4. kudharau wengine [   ]

2. Oanisha fungu A na fungu B ili kupata maana kamili

Fungu A

Fungu B

(i). Tukio la kihistoria [   ]

(ii). Kumpa pole rafiki yako aliyejikwaa [   ]

(iii). Kufanya kazi kwa ushirikiano [   ]

(iv). Kusema uongo [   ]

A. Tendo la huruma

B. Tendo lisilo la maadili

C. Uhusiano mwema

D. Mwaka wa kuzaliwa

 3. Jaza nafasi zilizo wazi kwa kuchagua neno kwenye mabano

(i). Kusaidiana katika jamii huleta ................................................. (umoja na mshikamano/chuki)

(ii). Kusalimia wakubwa ni tendo la ........................................................................... (adabu/huruma)

(iii). Kupigana shuleni ni tendo la ............................................................................... (upendo/ukatili)

(iv). Historia huelezea matukio ............................................................................ (yajayo/yaliyopita)

4. Chunguza matendo kwenye jedwali lifuatalo kisha weka alama ya vema (√) kwenye sehemu inayohusika kuainisha kama ni tendo linalofaa au lisilofaa.

Tendo

Tendo linalofaa

Tendo lisilofaa

(i). Kuwasalimia wazazi

 

 

(ii). Kuiba matunda

 

 

(iii). Kuomba msamaha unapokosea

 

 

(iv). Kutukana wenzako

 

 

5. Soma habari kisha jibu maswali

Vyanzo vya taarifa za Historia ya Tanzania ni vitu mbalimbali vinavyotuwezesha kupata taarifa za matukio yaliyowahi kitokea hapa nchini. Vyanzo hivyo ni kama kusikiliza masimulizi, kusoma vitabu na makumbusho ya Taifa. Vyombo vya habari na tovuti vinaweza pia kuwa ni vyanzo vya kupata taarifa za kihistoria. Vyanzo vya taarifa ya Historia ya Tanzania hutusaidia kupata taarifa za matukio yaliyowahi kutokea katika nchi yetu. Mfano wa tukio la kihistoria ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ulifanyika tarehe 26 Aprili 1964.

MASWALI

(i). Je, ni upi umuhimu wa vyanzo vya taarifa za historia ya Tanzania? . . . . . . . . . . . . ...

(ii). Chanzo cha taarifa za historia ya Tanzania ambacho huhusisha mazungumzo ya mdomo kinaitwajwe? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

(iii).Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulifanyika lini? . . . . . . . . . . . . . . . . . . ... . . .

(iv). Taja vyanzo viwili tu vya historia ya Tanzania. 

(i) . . . . . . . . . .. . .. ii. . . . . . . . . . .....

6. Tizama picha ifuatayo, kisha jibu maswali

image

 (i).Picha hiyo inaonesha mazingira ya wapi? . . . . . . . . . . . . . . . ...

(ii).Je, ni akina nani unawaona kwenye picha hiyo? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

(iii).Hao Watoto unaowaona kwenye picha wamesimama. Unadhani kwanini wamesimama? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...

(iv).Unafikiri tendo wanalolitenda kwa kusimama ni la heshima au dharau? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ..

LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD THREE EXAM SERIES 102

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUJIPIMA KWA SHULE ZA MSINGI 

MACHI 2025

DARASA LA TATU HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

 

  1. Tumia maneno yafuatayo kujaza swali la 1 hadi 5 

 

  1.   Raisi wa kwanza wa Tanganyika alikua anaitwa 
  2.  Kabla ya mungano Tanzania ilikua inaitwa 
  3. Kusaidiai kuwatunza, kuwatharnini na kuwalea wazee ni  
  4. Taifa la kwanza kuitawala na kufanya koloni lake Tanganyika 
  5.  Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 na kuunda jamuhtiriya

2. Andika majibu matendo yasiyofaa au yanayofaa 

i. Kutokupenda kufanya kazi  

ii. Kuwahi shuleni  

iii. Kuchelewa kurudi nyumbani  

iv. Kutoroka shuleni 

v. Kuwasaidia wasiojiweza  

3. Toa majibu katika maswali yafuatayo 

i.  Historia ya Tanzania ni elimu kuhusu matukio yaliyojitokea nchini 

ii. Maadili ni nini?  ……………………….

iii. Historia inaweza kuhusu maisha yetu binafsi, familia au ………………

iv. Raisi wa awamu ya pili wa Jamuhuri ya muungano alikuwa anaitwa………… 

v. Kuwasaidia mzigo watu wazee ni miongoni mwa matendo  katika jamii ………………..

SEHEMU B: 4. JIBU NDIYO AU HAPANA 

i. Kuwathamini na kuwalea wazee ni matendo ya kimaadili 

ii. Kuwaheshimu watu waliokuzidi umru sio jambo la kimaadili 

iii. Kusema ukweli ni jambo la kimaadili   

iv. Sehemu mojawapo ya vyanzo vya historia ya Tanzania ni makumbusho ya taifa  

v. Kuwanyanganya na kuwadhalilisha ni jambo la kimaadili 

 

LEARNINGHUBTZ.CO.TZHISTORIA STANDARD THREE EXAM SERIES 99

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256