FORM FOUR KISWAHILI NECTA 2025

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA 

MTIHANI WA KUHITIMU KIDATO CHA NNE 

KISWAHILI

(Kwa watahiniwa Walioko na Wasiokuwa Shuleni)

Muda: Saa 3 Mwaka: 2025

Maelekezo

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na moja (11).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali mawili (2) kutoka sehemu C ambapo swali la tisa (9) ni la lazima.
  3. Sehemu A ina alama kumi na sita (16), sehemu B alama hamsini na nne (54) na sehemu C ina alama thelathini (30).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na ya kila swali.
  5. Majibu yote yaandikwe kwa kalamu yenye wino wa bluu au mweusi.
  6. Vifaa vya mawasiliano na vitu visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  7. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia.

SEHEMU A (Alama 16)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

1. Katika vipengele (i) hadi (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika kijitabu chako cha kujibia.

(i) Ni taarifa zipi zinazoandikwa kupatikana katika kamusi kati ya hizi?

  1. Neno, maana, matumizi na matamshi ya semi
  2. Maana, neno, mazungumzo na matumizi ya semi
  3. Matamshi ya semi, matamshi, maana na mazungumzo
  4. Matamshi, mazungumzo, maana na kidahizo
  5. Kidahizo, matamshi, mazungumzo na semi
Choose Answer :


(ii) “Juma anaendesha baiskeli yake polepole.” Kiarifu cha sentensi hii kimejengwa na mfuatano upi wa vipashio?

  1. Kiima, chagizo na shamirisho
  2. Kitenzi kshirikishi, shamirisho na chagizo
  3. Kiarifu, kiima na chagizo
  4. Shamirisho, chagizo na kitenzi kikuu
  5. Kitenzi kikuu, shamirisho na chagizo
Choose Answer :


(iii) “Tutakuja kumpokea kwenye uwanja wa ndege.” Kazi ya kielezi kinachojitokeza kwenye sentensi hii ni ipi kati ya hizi?

  1. Kueleza idadi
  2. Kueleza mahali
  3. Kueleza namna
  4. Kueleza wakati
  5. Kueleza nafsi
Choose Answer :


(iv) Tamathali ipi ya semi hufanisha mambo kwa kutumia viunganishi?

  1. Tashititi
  2. Sitiari
  3. Nidaa
  4. Tashbihi
  5. Tabaini
Choose Answer :


(v) Tamathali ipi ya semi inatawala katika wimbo ufuatao?

Ze ndi ndi ndi! 

Tolly ndi! 

Ndi ndi ndi ndi! 

Tolly ndi! ×4

  1. Tabaini
  2. Taniaba
  3. Tashbihi
  4. Takriri
  5. Tashihisi
Choose Answer :


(vi) Neno lipi linadhihirisha kauli ya kutendeka katika kitenzi pika?

  1. Pikia
  2. Pikiwa
  3. Pikika
  4. Pikwa
  5. Pikisha
Choose Answer :


(vii) Yupi kati ya watafiti wanaojishughulisha na kusoma, kuchambua na kutoa maoni katika kazi za sanaa?

  1. Mdhamini
  2. Mtunzi
  3. Mhariri
  4. Msomaji
  5. Mhakiki
Choose Answer :


(viii) Hatua mojawapo ya uendelezaji wa lugha ili itumike kitaifa na kimataifa ni kuisanifisha. Jambo lipi kubwa linalofanywa katika hatua hii kati ya yafuatayo?

  1. Kupunguza maneno ya kukopa
  2. Kuondoa tofauti za kimsamiati
  3. Kuifanya itumike na jamii ndogo
  4. Kuweka tofauti za kimatamshi
  5. Kuidhinisha tofauti za maneno
Choose Answer :


(ix) Ni kwa namna gani tungo hutofautiana na sentensi?

  1. Tungo zote ni sentensi lakini sentensi zote si tungo
  2. Sentensi haitoi taarifa kamili lakini tungo hutoa taarifa kamili
  3. Sentensi ni miongoni mwa tungo lakini si kila tungo ni sentensi
  4. Tungo sharti ikamilike lakini sentensi si lazima ikamilike
  5. Tungo ni ndefu sana lakini sentensi ni fupi sana
Choose Answer :


2. Oanisha mifano ya tamathali za semi iliyo katika Orodha A na tamathali husika zilizo katika Orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kijitabu chako cha kujibia.

Orodha A
Orodha B
  1. Kilio cha mama mfiwa kilisikika mithili ya king’ora.
  2. Haba na haba hujaza kibaba.
  3. Misitu ni uhai.
  4. Shughuli zimejifungua salama.
  5. Upepo mkali ulipiga mluz(i) kila ulipogonga kingo za mito.
  6. Binadamu hupanga, Mungu hupanga.
  1. Majazi
  2. Tashihisi
  3. Tashinda
  4. Tabaini
  5. Tashbihi
  6. Onomatopoea
  7. Sitiari
  8. Takriri
View Ans


SEHEMU B (Alama 54)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3.(a)Tumia mzizi chez- kuunda vitenzi viwili kwa kila kauli kama zilivyoorodheshwa: 

  1. Kauli ya kutendana 
  2. Kauli ya kutendeka 
  3. Kauli ya kutendea 
  4. Kauli ya kutendewa

(b) Unda nomino moja kwa kila kitenzi.

  1. Zaa
  2. Kimbia
  3. Shikilia
  4. Elekeza
  5. Penda
View Ans


4.(a) Fafanua viyanzo vinne vya misimu kwa kutoa mfano mmoja kwa kila chanzo cha misimu husika.

(b) Eleza maana mbili kwa kila neno.

  1. Kaka
  2. Kito
  3. Mkaa
  4. Mkwaju
  5. Babu
View Ans


5. Bainisha viambishi vya o - rejeishi katika kila sentensi kwa kuvipigia mstari kisha taja ngeli husika kwa kila kirejeishi. 

  1. Udongo ulioleta umeauka
  2. Kioo kilichovunjika kimeletwa 
  3. Karatasi zilizokauka zimetumika 
  4. Mlimokuwa na joto sana 
  5. Kijana atakayeshinda atapewa zawadi
  6. Gazeti lilichapwa limekwisha
  7. Barabara iliyofunguliwa imekamilika
  8. Magonjwa yaliyowasumbua yalikokana na athari ya mvua
  9. Ng’ombe aliyemkungia shimoni amekolewa 
View Ans


6. Eleza kwa kifupi maana na nahau zifuatazo: 

  1. Juma ana mkono wa birika 
  2. Kaka amepata jiko 
  3. Mjomba amepiga maji 
  4. Mwezi amekata mgongo 
  5. Mtoto amevimba kichwa 
  6. Beka ana mkono mrefu 
  7. Rafiki yangu anazaka kamba 
  8. Kijana amepiga kete 
  9. Huyu dada amepiga mbichi 
View Ans


7. Eleza kwa kifupi sifa sita zilizokifanya Kiunguja kusanifishwa na kuwa lugha sanifu ya Kiswahili. 

View Ans


8. Soma kifungu cha habari kifuatacho kisha jibu maswali yanayofuata. Kwa hakika mwaka ule watu walinuna sana. Haikuwahi kutokea karibuni kwa kipindi cha muongo mmoja hivi kuwa na mvutano wa kisiasa hicho. Maghala yalijaa mahindi, mtama, mpunga, uwele, maharawe, njegere na njugumawake. Nyama nyingi ziliileta kutoka porini ambapo wanawake walizisanda na kuzikauusha motoni. Aidha, samaki wakubwa wakubwa walipatikana kwa wingi, samaki ambao hawakuwahi kupatikana hapo awali. Kila mmoja kijijini hapo alikuawa na furaha. 

Mavuno hayo yaliambatana na sherehe za mwisho wa mwaka ambazo zilikuwa ni zenye kufurahisha. Vigelegele vilisikika, ngoma zilipigwa na marimba yakavuma kijijini huku watu wa rika zote wakicheza bila kujali kuwa ni wazee au watoto. Wasichana wa umri wa miaka kulekulea kumi na mbili walitikisa miili yao kwa mvuto, huku miguu yao ikifuata mitindo maalumu kutoka andani ngoma yenye vumbi, wakicheza kwa madaido wakizungusha shingo zao kama twiga mbugani. Walipeana zamu ya kucheza wengine wakiwa wawili na wengine watatuwatu. Baadaye, wavulana nao waliwezaa ngoma yao. Kadiri ngoma zilivyoundwa, ndivyo vijana waliwyokuwa wakicheza na kuruka juu kama swala. Wazee walitazama na kuridhika huku wanawake wakishangilia kwa vigelegele wakati vijana walioishiwa pumzi wakiondoka jukwaani. 

Wakati wanawake na vijana wakicheza na kuimba, wazee walileta kando ya moto wakinywa sharubati mpya. Mmoja baada ya mwingine, wazee hao walisisimama na kuanza kucheza. Wakaijarisha vija kwa mara nyingi tena. Inaga hawakuwa na kasi kama vijana, lakini waliwapiku katika mvuto na ubunifu wa uchezaji wao. 

Wapigaji watatu wa marimba walijitokeza na kuonyesha umahiri wao. Kila mpigaji alionesha uhodari wake wa kupiga marimba, kuimba na kucheza. Alipoacha, mwingine alijitokeza, akiimba na kujiunga na tungo iliyoanzishwa. Walikuwa kama kundi la muziki wa wapiga marimba ambao kila aliyekasikia alitviwa na upigaji wa marimba yao uliomliza moyo wa mwayo hadi ndani ya moyo wake. Pangoni. Mdondo wa mziki wa marimba uliingia mwilini mwa mmoja hadi ndani ya moiyo yao. 

Wakati wa machweo, watu walipunzwa na kula chakula. Wapiga marimba waliungana na wapiga ngoma na huku na nyimbo za huo uchezi uliendelea tena hadi usiku wa manane. Kilichowandoa watu uwanjani pale ni ama uchovu au usingizi.

Maswali

(a) Andika kichwa cha habari uliyoisoma kisichopungua maneno matatu na kisichozidi maneno matano.

(b) Bainisha shughuli mbili muhimu zilizokuwa zikiwapitia watu riziki kulingana na habari uliyoisoma.

(c) Fafanua kwa kifupi maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika habari uliyoisoma:

  1. Muongo mmoja
  2. Walivapipiku

(d) Fupisha habari hii kwa maneno yasiyopungua mia moja (100) na yasiyozidi mia na tano (105).

View Ans


SEHEMU C (Alama 30)

Jibu maswali mawili (2) kutoka katika sehemu hii. Swali la tisa (9) ni la lazima na kila swali lina alama 15.

9. Jifanye wewe ni mmojawapo wa watoto waliohudhuria kongamano lililohusu haki za watoto. Andika beti tano za utenzi kuhusu “Haki za Mtoto.”

View Ans


ORODHA YA VITABU 

RIWAYA 

  • Takadini   -   Ben J. Hanson (MBS) 
  • Watoto wa Mama N’tilie   -   E. Mbogo (H.P) J
  • oka la Mdimu     -   A. J. Safari (H.P)

TAMTHILIYA 

  • Orodha   -   Steve Reynolds (MA) 
  • Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe   -   E. Semzaba (ESC) 
  • Kilio Chetu -   Medical Aid Foundation (TPH)

10. Lengo kuu la kazi za fasihi ni kuonya na kuisaza jamii. Thibitisha kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila riwaya kutoka katika riwaya mbili ulizosoma. 

View Ans


11. “Uzembe ni jambo linalokwamisha maendeleo ya jamii nchini Tanzania.” Tathmini kauli hii kwa kutoa hoja tatu kwa kila tamthiliya kutoka katika tamthiliya mbili ulizosoma.

View Ans





Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256