HISTORIA YA TZ NA MAADILI FORM TWO REGIONAL EXAMS (MOCK, PRE-NATIONAL, etc.)

Namba Ya Upimaji ____________________

OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

image 

MTIHANI BAADA YA MTIHANI WA UTAMIRIFU KIDATO CHA PILI MKOA WA KILIMANJARO

 060 HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

Masaa 2:30 Ijumaa Tarehe 19 Septemba, 2025

MAELEKEZO

  1. Mtihani huu una sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa
  3. Sehemu A na C zina alama kumi na tano (15) kila moja na sehemu B ina alama sabini (70)
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali.
  5. Andika namba yako ya usajili katika kila kurasa
KWA MATUMIZI YA WATAHINI TU
NAMBA YA SWALI ALAMA SAHIHI YA WATAHINI
1

2

3

4

5

6

7

8

9

10

JUMLA

SAHIHI YA WAHAKIKI

SEHEMU A (ALAMA 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Katika kipengele (i) hadi (x) chagua herufi ya jibu sahihi, kisha Andika herufi ya jibu hilo katika kisanduku ulichopewa.

i. Mwanafunzi mgeni wa kidato cha kwanza aitwae Meko ameshindwa kuelewa kwa undani maana ya neno “Historia ya Tanzania”.Mwalimu wa somo hilo Rashidi akakupa nafasi ya kumuelewesha kwa ufupi. Ipi katiya maana zifuatazo utazizingatia wakati wakumuelewesha?

  1. Ni jumla ya matukio yatakayotokea nchini Tanzania nakuleta athari katika nyanja mbalimbali.
  2. Ni jumla ya matukio yaliotokea Tanzania kati ya mwaka 1961 hadi hivi leo.
  3. Ni jumla ya matukio yaliyotokea nchini Tanzania nakuleta athari katika nyanja mbalimbali.
  4. Ni jumla ya matukio yaliyotokea duniani yenye athari kiuchumi, kijamii na kitamaduni.

ii. Salma anajivunia kuwa miongoni mwa wanafunzi wanaosoma somo la “Historia ya Tanzania naMaadili”, kwa kuwaelimisha kuwa na mapenzi na nchi yake. Kitendohiki cha Salma kuipenda nchi yake kinajulikana kuwa ni?

  1. Amani 
  2. Utu 
  3. Ukarimu
  4. Uzalendo

iii. Wakati wa ufundishaji wa mada ya pili katika dhana ya jamii, Mwalimu Juma alisema “Ni mkusunyiko wa familia mbalimbali zenye uhusiano wa karibu” Maana hii ina shabihiana na ipi kati ya vipengele vifuatavyo?

  1. Kabila 
  2. Ukoo 
  3. Jamii
  4. Taifa

v. Katika kuhakikisha utunzwaji wa maeneo ya kihistoria duniani, Umoja wa Taifa umeunda shirika linaloshughulikia utambuzi na upitishaji wa maeneo hayo kama Urithi wa dunia na nchi husika. Lipi kati ya mashirika yafuatayo linajihusisha na maswala tajwa hapo juu?

  1. UNICEF 
  2. ILO 
  3. UNESCO
  4. UNHCR

vi. Mila, desturi, lugha na ufundi ni kundi linalowakilisha Urithi unaopatikana katika nchi ya Tanzania, Je ni aina gani ya urithi?

  1. Urithi wa Taifa 
  2. Urithi wa Asili 
  3. Urithi unaoshikika
  4. Urithi usioshikika

vii. Katika hotuba yake juu ya ustawi wa maadili na maliasili za taifa, Waziri mkuu alizungumzia majukumu yanayohusiana na uhifadhi na ulinzi wa Urithi wa taifa na maadili. Unadhani ni nani haswa anayehusika na ulinzi huo kwa maendeleo ya taifa letu?

  1. Rais wa Tanzania 
  2. Mkuu wa majeshi 
  3. Kila mtanzania
  4. Afisa maliasili

viii. Waarabu wa kwanza kuja Pwani ya Afrika walikuja kufanya biashara ya

  1. Pembe za ndovu na watumwa 
  2. Karafuu na mbogamboga abiria
  3. Pembe za ndovu na kusafirisha
  4. Nazi na vilevi

ix. Mfumo wa utawala wa waingereza ulibadilika kutoka

  1. Uwakala kwenda moja kwa moja 
  2. Moja kwa moja kwenda uwakala 
  3. Uwakala
  4. Moja kwa moja

ix. Misingi mikuu ya maadili ya jamii za Kitanzania wakati wa ukoloni unaingia umejipambanua katika Nyanja mbalimbali ikijumuisha vipengele vifuatavyo isipokua kipengele kimojawapo:-

  1. Mila na desturi 
  2. Michezo na sanaa za kuigiza 
  3. Utawala wa jadi
  4. Lugha na mawasiliano

x. Sababu zilizopelekea kushindwa kwa jamii nyingi za Kitanzania katika kupambana na ukoloni ni pamoja na :-

  1. Matumizi ya silaha duni 
  2. Umoja na mshikamano 
  3. Imani potofu dhidi ya mkoloni
  4. Kukosekana kwa muamko wa wananchi

MAJIBU

i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x











2. Oanisha vipengele vinavyoonesha kauli na kampeni za maraisi wa Tanzania katika vipindi mbalimbali juu ya mapambano dhidi ya rushwa na mmomonyoko wa maadili kutoka Orodha A na kundi husika kutoka Orodha B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa.

ORODHA A

ORODHA B

  1. African Association (AA)
  2. Tanganyika African Association (TAA)
  3. Afro- Shirazi Party (ASP)
  4. Zanzibar and Pemba People’s Party (ZPPP)
  5. Zanzibar Nationalist Party (ZNP)
  1. 1957 
  2. 1955 
  3. 1929 
  4. 1948
  5. 1959

MAJIBU

i

ii

iii

iv

v






.

SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

3. Kileo ni mwanafunzi wa kidato cha pili aliyeshindwa kuelewa athari mbalimbali za mifumo ya wakoloni katika maadili ya Kitanzania, muelezee athari zifuatazo

  1. Elimu
  2. Afya
  3. Dini za jadi
  4. Lugha
  5. Mavazi

4. Wanafunzi wa mkondo wa bishara wa shule ya sekondari Mawella walitakiwa kufanya utafiti kwa njia ya mtandao ili kubaini shughuli mbali mbali zilizofanywa na makundi ya Jamiii ya asili ya Kitanzaniaa . Unadhani ni shughuli zipi walizibaini na kuzinukuu katika madaftari yao? (Taja shughuli tano (5) ).

5. Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar walitumia mbinu mbalimbali za kudai uhuru, onesha mbinu tano (5) zilizotumika kupigania uhru kutoka kwa wakoloni.

6. Jamii za Kitanzania imebeba zana ya kuwa na tabia, Ziainishe tabia tano (5) njema zinazofanywa na Watanzania.

7. Chriss ni mwanafunzi wa chuo cha Oxford nchini Uingereza, anapenda umjulishe orodha ya urithi (5) wa dunia upatikanao Tanzania

8. Mwalimu wa somo la Historia ya Tanzania alifundisha juu ya fursa zitokanazo na urithi wa jamii za Kitanzania ambapo alianisha mambo mbalimbali. Taja fursa tano (5)

9. Taja makundi makuu matano ya jamii za jamii za kitanzania.

Sehemu C (Alama 15)

Jibu swali la kumi (10).

10. Sokomoko ni kijana asiye na maadili katika jamii,wewe kama kijana mwenzake mfundishe juu ya faida ya maadili katika jamii,toa hoja sita (6).

FORM TWO HISTORIA EXAM SERIES 151  

FORM TWO HISTORIA EXAM SERIES 151  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256