FORM ONE HISTORIA EXAMS SERIES

JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA RAIS – TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI

KIDATO CHA KWANZA

MUDA: SAA 2:30  2025

MAELEKEZO

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi (10).
  2. Jibu maswali yote kwenye sehemu ulizopewa.
  3. Sehemu A na C zina alama kumi na tano (15) kila moja na sehemu C alama sabini (70).
  4. Zingatia maelekezo ya kila sehemu na kila swali
  5. Andika namba yako sahihi uliyosajiliwa nayo

SEHEMU A (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

1. Katika vipengele (i) – (x), chagua herufi ya jibu sahihi kisha andika herufi ya jibu hilo katika visanduku ulivyopewa.

(i) Bibi Halima alishuhudia baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha madongo wakitupa taka katika vyanzo vya maji. Katika kutimiza wajibu wake aliwaeleza kuwa wanaharibu urithi wa taifa. Urithi uliokusudiwa na bibi Halima unaingia katika kipengele kipi kati ya vifuatavyo?

  1. Urithi usioshikika
  2. Urithi wa asili
  3. Urithi unaoshikika
  4. Urithi wa kale.

(ii) Ulinzi wa Historia ya Tanzania ni jukumu la kila Mtanzania mwenye mapenzi mema na Taifa hili la Tanzania. Ipi ni njia bora na sahihi ya kulinda historia ya Tanzania?

  1. Kufuta mila za jadi
  2. Kurekodi kumbukumbu
  3. Kuharibu maeneo ya kihistoria
  4. Kuiga tamaduni za kigeni.

(iii) Nyimbo na ngoma za jadi huimbwa na kupigwa kwa makusudi makubwa kabisa. Ni kipi kati ya yafuatayo huimarishwa pale ngoma na nyimbo zinapohusishwa?

  1. Teknolojia
  2. Maadili ya jamii
  3. Ubaguzi wa kijamii
  4. Mazoea ya kigeni

(iv) Michoro inayochorwa maeneo mbalimbali ya kuhistoria ina makusudi makubwa katika nchi yetu ya Tanzania. Nini nia kubwa ya kuchora picha maeneo ya kihistoria?

  1. Kujitafutia umaarufu 
  2. Kukuza maadili 
  3. Kuhifadhi urithi
  4. Kujaribu uchoraji

(v) Nyimbo za jadi huimbwa na makabila mbalimbali hapa nchini Tanzania. Je! Ni wakati gani unaofaa kuimba nyimbo hizi za jadi?

  1. Skukuu za kidini tu
  2. Tamasha la kisiasa
  3. Shughuli za kijadi kama harusi
  4. Maonesho ya magari

(vi) Katika hotuba yake juuya ustawi wa maadili na maliasili za taifa, waziri mkuu alizungumzia majukumu yanayohusiana na uhifadhi na ulinzi wa urithi wa taifa na maadili. Unadhani ni nani hasa anahusika na ulinzi huo wa maendeleo ya taifa letu?

  1. Rais wa Tanzania
  2. Mkuu wa majeshi
  3. Kila mtanzani
  4. Afisa maliasili

(vii) Mabadiliko gani yamekuwa yakizingatiwa katika historia ya Tanzania?

  1. Mabadiliko ya hali ya hewa
  2. Mabadiliko ya teknolojia pekee
  3. Mabadiliko ya kijamii, kisiasa na kiuchumi
  4. Mabadiliko ya michezo

(viii) Makundi katika jamii za Kitanzania hujishughulisha na shughuli mbalimbali ambazo huwapatia kipato. Ipi si shughuli ya wanilo kati ya hizi zifuatazo?

  1. Ufugaji 
  2. Uwindaji 
  3. Kilimo
  4. Uvuvi 

(ix) “Kupokea au kutoa mali isiyo halali au kutumia mali ya umma isivyo halali kwa manufaa binafsi.” Maelezo haya yanahitimishwa na neno lipi kati ya haya yafuatayo?

  1. Ukoloni
  2. Takrima 
  3. Rushwa
  4. Udhalimu 

(x) Watanzania wote bila kujali kabila, imani, rangi na dini hatunabudi kuzingatia miongozo, kanuni na sheria zinazoongoza mienendo ya mtu mmoja mmoja katika nchi yetu. Lipi ni jina moja linalojumuisha miongozo hiyo?

  1. Mila 
  2. Desturi
  3. Utamaduni
  4. Maadili

MAJIBU

i

ii

iii

iv

v

vi

vii

viii

ix

x











2. Oanisha sentensi kutoka kundi A na zile za kundi B, kisha andika herufi ya jibu sahihi katika kisanduku ulichopewa hapo chini.

KUNDI A

KUNDI B

(i) Njia ya kuhifadhi historia ya jamii

(ii) Mfano wa maadili ya kitanzania

(iii) Michezo ya jadi

(iv) Namna ya kuhifadhi urithi wa taifa

(v) Umuhimu wa kulinda na kutunza historia ya taifa

  1. Kuchora alama za urithi
  2. Kusaidiana na kuheshimu wengine
  3. Bao na rede
  4. Kuandika kumbukumbu
  5.    Kuweka kumbukumbu kwa vizazi
  6.    Kusoma na kuandika
  7. Kujifunza mara kwa mara

KUNDI A

i

ii

iii

iv

v

KUNDI B






SEHEMU B (Alama 70)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Taja shughuli tano (5) za kijamii na kiuchumi zinazofanywa na jamii ya wakichembe katika maisha yao ya kila siku.

  1. __________________________________________________________________
  2. __________________________________________________________________
  3. __________________________________________________________________
  4. __________________________________________________________________
  5. __________________________________________________________________

4. (a) Eleza maana ya urithi wa Taifa

________________________________________________________________________________________________________________________________________________

(b) Taja njia nne (4) zinazotumika kuhifadhi urithi wa taifa:-

i) ______________________________________________________________________

ii) ______________________________________________________________________

iii) _____________________________________________________________________

iv) _____________________________________________________________________

5. (a) Taja michezo miwili ya jadi inayotumika kuendeleza maadili

  1. _________________________________________________________________
  2. _________________________________________________________________

(b) Eleza namna michezo hiyo inavyosaidia watoto kujifunza maadili.

i) ______________________________________________________________________

ii) ______________________________________________________________________

iii)______________________________________________________________________

6. Bainisha mifano mitano ya maadili mbalimbali katika jamii za Kitanzania ambayo ingefaa kuigwa na kudumishwa kwa vizazi vijavyo.

  1. __________________________________________________________________
  2. __________________________________________________________________
  3. __________________________________________________________________
  4. __________________________________________________________________
  5. __________________________________________________________________

7. (a) Bainisha makabila mawili (2) ambayo yanatokana na jamii za wakichembe.

  1. __________________________________________________________________
  2. __________________________________________________________________

(b) Taja zana tatu (3) zilizotumika katika uwindaji katika jamii ya Wakichembe.

i)  __________________________________________________________________

ii)  __________________________________________________________________

iii) __________________________________________________________________

8. Jamii za watu wa visiwa vya Zanzibar walinunua na kuuza bidhaa kupitia biashara walizofanya na waajemi, waarabu na watu wa mashariki ya mbali. Taja bidhaa tano (5) zilizohusika katika biashara hiyo.

  1. __________________________________________________________________
  2. __________________________________________________________________
  3. __________________________________________________________________
  4. __________________________________________________________________
  5. __________________________________________________________________

9. Kwa nini jamii za asili ya Kitanzania zilihama kutoka eneo moja kwenda eneo lingine? Toa hoja tano (5).

  1. __________________________________________________________________
  2. __________________________________________________________________
  3. __________________________________________________________________
  4. __________________________________________________________________
  5. __________________________________________________________________

SEHEMU C (Alama 15)

Jibu swali hili kwa insha

10. Eleza hoja sita (6) ukionesha matarajio yako ya kujifunza somo la Historia ya Tanzania na  Maadili.

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 203  

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 203  

OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

MTIHANI WA KUMALIZA NUSU MUHULA KIDATO CHA KWANZA

HISTORIA YA TANZANIA NA MAADILI 2025

MUDA 2:30

MAELEKEZO

1. Karatasi hii Ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi 10

2. Jibu maswali yote kwenye nafasi ulizopewa 

3. Sehemu A na C Zina alama kumi na Tano (15) Kila na sehemu B Ina alama sabini (70)

4. Zingatia maelezo ya Kila sehemu na ya Kila swali 

5. Andika jina lako juu ya karatasi hii.

 

SEHEMU A. Alama 15

1. Chagua jibu sahihi kutoka machuguzi uliopewa kwa vipengele (i)- (x) kasha andika jibu lake katika nafasi uliopewa.

i) Somo la historia ya Tanzania na maadili linaundwa na dhana kuu mbili nazo ni

  1. Historia ya Tanzania na maadili
  2. Historia kuhusu mambo au matukio yaliyopita
  3. Historia ya Tanzania na Tehama
  4. Historia ya Tanzania na utu

 ii) Ni miongozo inayotawala tabia na matendo ya mtu mmoja mmoja au jamii kwa ujumla. dhana hii imebebwa na neno

  1. Maadili
  2. Huruma
  3. Tanzania
  4. Historia

iii) Neno maadili linapotumika huweza pia kuashiria au kuimarisha Tunu za jamii au taifa ni zipi Kati ya zifuatazo

  1. Uhuru na Amani
  2. Amani na furaha
  3. Furaha na unyenyekevu
  4. Unyenyekevu na upendo

vi) Tunaweza kuwakaribisha wageni kwa furaha na kuwapa heshima kubwa ikiwa pamoja na kukirimiwa kwa 

  1. Chakula na malazi
  2. Chakula na malezi
  3. Chakula na kuoga
  4. Chakula na heshima

v) Mazingira ya kiliografia yanaweza kuathiri shughuli za binadamu kama vile 

  1. Biashara,utamaduni,kilimo na uhamaji wa watu
  2. Biashara,uchumi,siasa, na mazingira
  3. Uchumi,jamii,uvuvi, na uwindaji
  4. Uwindaji,ukusanyaji,ulinzi na mazingira

vi) Kwa kutumia uchambuzi wa makabila Tanzania ni nchi yenye makundi ya makabila yote yanayopatikana barani Afrika makundi hayo ni

  1. Wabantu ,wakichembe,wakushito na wanilo
  2. Wabantu,wangoni,wamakonde na wazaramo
  3. Wakichembe,Wabantu,wahaya na wanyakyusa
  4. Wanilo,wakushito,wakichembe,na wapemba

vii) Kihistoria kundi kubwa la tatu la watanzania ambalo ni jamii ya wafugaji walioingia nchini Tanzania wakitokea kusini mwa sudani ni 

  1. Wabantu
  2. Wanilo
  3. Wakushito
  4. Wakichembe

viii) Jamii za wakushito zinahusisha makabila kama 

  1. Wairaki,wagorowa, na waburugi
  2. Wamasai,wapare na Wairaki
  3. Wameru,Wamasai na Hadzabe
  4. Hadzabe,Tindiga, na Wairaki

ix) Kwa hapa Tanzania jamii za Wanilo ni kama 

  1. Wamasai,wajaluo, na wadatoga
  2. Wamasai Wairaki, na wadatoga
  3. Wadatoga,wajaluo na Hadzabe
  4. Hadzabe,Tindiga na Wairaki

x) Morani ni kundirika katika jamii ya kimasai la vijana wenye umri Kati ya miaka

A) 18 na 35

B)18 na 40

C)18 na 60

D) 18 na 80

 

2. OANISHA JIBU LA ORODHA 'A' NA JIBU LA ORODHA 'B'

ORODHA A

ORODHA B

  1.                     Wakichembe
  2.                   Wanilo
  3.                 Wabantu
  4.                 Mitala

 

  1. Hutumia lugha ya kugongagonga ulimi
  2. Wairaki na wagorowa
  3. Wadatoga na Wamasai
  4. Wahadimu,watumbatu na wapemba
  5. Ndoa za wake wengi

 

 

SEHEMU B. Alama 70

Jibu maswali yote katika sehemu hii

3. Mkude ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya wavulana buingu . Ameshindwa kuelewa maana ya maneno yafuatayo kwenye somo la historia ya Tanzania na maadili. Msaidie kumuelezea maana ya maneno hayo.

a) Tunu za taifa

b) maadili

c) Jiografia

d) Jamii

e) wajibu

4. Ukiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza mkondo A waelezee wanafunzi wenzako umuhimu wa kuwa na maadili katika jamii na taifa kwa ujumla.

5.Warioba ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza alichaguliwa na jamii yake kuelezea namna ambavyo vijana wanaweza kujengwa kwa kuwa na tabia njema. Msaidie warioba katika kuwaeleza vijana vitu vinavyojenga tabia njema katika jamii zetu nukta Tano.

6. Ukiwa Kama mwanafunzi kutoka shule ya sekondari chekeleni. waelezee wanafunzi wenzio kwanini jamii za Asili ya kitanzania zilihama kutoka eneo Moja kwenda eneo jingine nukta Tano

7. Kwa kutumia nukta Tano tofautisha jamii za Asili za wakichembe na jamii za Asili za kibantu.

8. Kwa kumtumia mtaalamu "EMILE DURKHEIM" (1884) Toa dhana ya neno 'Jamii'

9. Eleza Tofauti iliyopo Kati ya maadili yaliyojengwa katika jamii za Asili na jamii za sasa za kitanzania

SEHEMU C Alama 15

Jibu swali la kumi

Bainisha changamoto za kukuza maadili katika jamii unamoishi na Kisha toa mapendekezo ya jinsi ya kuzitatua.

 

 

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 201  

FORM ONE HISTORIA EXAM SERIES 201  

Download Learning
Hub App

For Call,Sms&WhatsApp: 255769929722 / 255754805256