OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA KUMALIZA MUHULA WA PILI
KIDATO CHA KWANZA
ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
Muda: Saa 2 Novemba, 2026
MAELEKEZO
| KWA MATUMIZI YA MTAHINI TU. | ||
|---|---|---|
| NAMBA YA SWALI | ALAMA | SAINI YA MTAHINI |
| 1. | ||
| 2. | ||
| 3. | ||
| 4. | ||
| 5. | ||
| 6. | ||
| 7. | ||
| 8. | ||
| 9. | ||
| 10. | ||
| JUMLA | ||
| SAINI YA MHAKIKI | ||
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
1. Katika kipengele (i) – (x), chagua jibu sahihi kisha andika herufi yake.
i. Kwanini elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?
Kuleta maendeleo katika jamii
Kutatua changamoto za wanadamu
Kufuata mwenendo wa Mitume (A.S)
Kumuabudu Allah (S.W) ipasavyo.
ii. Ni itikadi gani ya maisha iliyojengwa katika kujitenga na vitu vizuri na kumletea mwanadamu maendeleo miongoni mwa itikadi za dini?
Ukafiri
Utawa
Ushirikina
Upagani.
iii. Mtume Muhammad (S.A.W) alishushiwa aya tano za mwanzo akiwa katika pango la Hira. Aya hizi zinapatikana katika sura gani?
Surat Al – Faatih’a
Surat Al - Lahabi
Surat Al – A’laq
Surat Al – Falaq.
iv. Gomwa Mponda na wenzie wamekuwa na ubishani juu ya mgawanyo wa elimu katika uislamu hasa elimu ambayo ni faradhi ‘Ain. Ni ipi elimu ambayo ni Faradhi ‘Ain kati ya hizi?
Elimu ya Mazingira
Elimu ya Mwongozo
Elimu ya Akhera
Elimu ya Dunia
v. Qur’an ni kitabu cha Allah (S.W) kilichoteremshwa kwa ajili ya wanadamu wote. Bainisha kusudio la kuteremshwa kitabu hiki.
Kusomwa mara kwa mara katika swala
Kuongoza maisha ya mwanadamu
Kufukuzia majini na mashetani
Kuhifadhiwa katika vifua vya Waislamu.
vi. Bainisha sura inayowafunza Waislamu adabu za kuomba dua kwa Allah (S.W).
Surat Al – Ikhlas’
Surat Annas
Surat Al – Faatih’a
Surat Al – Maau’n.
vii. “Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano”. Ni ipi nguzo ya Nne ya uislamu?
Kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani
Kutoa Zakat
Kusimamisha Swala
Kuhiji Makkah kwa mwenye uwezo.
viii. Kwa sababu gani ni muhimu kufuata Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W)?
Sunnah ni sehemu ya Qur’an tukufu
Huwezi kuitekeleza Qur’an ipasavyo bila Sunnah
Kuacha Sunnah ni sababu ya kupata dhambi
Sunnah ni sababu ya kuingia peponi.
ix. Muislamu analazimika kutekeleza swala tano za faradhi katika maisha yake. Bainisha kusudio la swala hizi.
Kinga ya maovu na machafu
Tiketi ya kuingia peponi
Kupata thawabu na heshima
Kumtambulisha Muislamu.
x. Kwa nini Waislamu wanafunga mwezi wa Ramadhani?
Kutafuta Ucha Mungu
Kufutiwa dhambi
Kuingia peponi
Kudumisha historia.
2. Oanisha maelezo kuhusu shahada katika orodha A na istilahi husika kutoka katika orodha B kisha andika herufi ya jibu sahihi kwa kila kipengele katika karatasi yako ya kujibia.
| Orodha A | Orodha B |
|---|---|
|
|
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
3. Imani ya kweli ya Muislamu inakamilika kwa kuzingatia mambo sita ya msingi sana kwa kila muumini. Orodhesha mambo hayo katika mpangilo sahihi.
4. (a) Kwa kuzingatia Sheria, nini maana ya Shahada?
(b) Mtume Muhammad (S.a.W) anatufundisha kuwa shahada ya kweli imegawanyika katika hatua kuu tatu, bainisha sehemu tatu za shahada.
5. (a) Janaba ni nini kisheria?
(b) Kwa kurejea kutoka katika Qur’an (4:43), taja mambo manne yaliyoharamishwa kufanya kwa mwenye janaba.
6. Surat Al – Fatihah ni sura inayosomwa mara kwa mara na hasa katika ibada ya swala. Fafanua kwa ufupi mafunzo manne ya sura hii.
7. (A) Mitume na Manabii wa Mwenyezi Mungu walitumia mbinu mbalimbali katika kuwalingania watu wao. Ni mbinu zipi walizozitumia katika kuwalingania watu wao?
(B) Ndani ya Qur’an Tukufu imetaja na kuelezea Mitume ishirini na tano. Wewe kama msomaji wa kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu (Qur’an) taja Mitume kumi na mbili waliotajwa ndani ya kitabu hicho.
8. Baadhi ya Waislamu wanapuuza Sunnah ya Mtume Muhammad (S.A.W) kwa kudai kwamba ukiitekeleza unapata thawabu na ukiicha hupati dhambi. Wabainishie hasara nne watakazopata duniani na akhera kutokana na mwenendo huu.
9. Kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W), Muislamu bora ni yule mwenye tabia njema na mwenye kuepuka tabia mbaya. Bainisha tabia mbaya tano utakazoziepuka katika maisha yako ya kila siku.
SEHEMU C (Alama 15)
Jibu swali la kumi (10).
10. “Lengo kuu la kusimamisha swala ni kumtakatisha mja kutokana na mambo maovu na machafu.” Qur’an (29:45). Kwa kuzingatia aya tajwa fafanua kwa utaratibu sharti nne (4) za kusimamisha swala. Wabillah Tawfeeq
FORM ONE EDK EXAM SERIES 307
FORM ONE EDK EXAM SERIES 307
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
MTIHANI WA NUSU MUHULA
KIDATO CHA KWANZA
021 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU
Muda Saa: 2:30 Septemba, 2026
Maelekezo
SEHEMU A (ALAMA 15)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
1. Chagua jawabu sahihi kisha Andika herufi ya jawabu katika kitabu chako cha kujibia
(i) Kwa mujibu wa uislamu, mtu aliye elimika anajitofautisha na wasioelimika kwa sifa hii
(ii) Hutokea iwapo Nun-sakinah na Tanwiin zitakuja kabla ya herufi sita za idh-haar
(iii) Katika uislamu kufuata sunnah ni utekelezaji wa shahada ya pili . Ni ipi kati ya zifuatazo ni dhana sahihi kuhusu sunnah?
(iv) Jambo gani ni lazima kutekeleza katika mchakato wa kumuosha maiti
(v) Wahyi wa kwanza kumshukia Mtume (S.A.W) ulisisitiza juu ya jambo gani
(vi) Bwana Bakari anajizuia na vyakula vizuri, anavaa nguo chakavu na kuishi katika nyumba isiyo na sakafu, akiamini kuwa kufanya hivyo ni kujikurubisha zaidi kwa Mungu . Bwana Bakari atakuwa ameathiriwa na mfumo gaani wa maisha?
(vii) Mwanaadamu analazimika kuisoma Qur’an kwa kuzingatia lengo kuu. Ni lipi lengo la kitabu hicho ?
(viii) Ni nguzo ya tano miongoni mwa nguzo za Uislamu ambayo hufanywa katika miezi maalum kwa mwenye uwezo
(ix) Sentensi ipi inabainisha njia zilizotumika kuhifadhi Qur’an wakati wa Mtume (S.A.W)
(x) Hadithi ndio njia kuu inayotumika kuhifadhi sunnah ya Mtume (S.A.W) Katika zama hizi. Ni ipi kati ya dhana zifuatazo ni sahihi kuhusu hadithi
MAJIBU
| i | ii | iii | iv | v | vi | vii | viii | ix | x |
| . |
2. Oanisha nyakati mahsusi za swala kulingana na mwenendo wa jua katika orodha A na majina ya swala zinazotekelezwa katika nyakati hizo katika orodha B kisha Andika herufi ya jawabu sahihi kwa kila kipengele.
| ORODHA | ORODHA B |
|
|
MAJIBU
| ORODHA A | i | ii | iii | iv | v |
| ORODHA B |
SEHEMU B (Alama 70)
Jibu maswali yote katika sehemu hii
3. Aya zifuatazo za suratul-Ikhlasw (112:1-4) zimechanganywa . Pangilia kwa usahihi kama ilivyoshuka katika Qur’an.
4.a) Allah anasema “Na anayetaka dini nyengine isiyokuwa Uislamu basi haitokubaliwa kwake. Naye akhera atakuwa katika wenye khasara” Qur’an (al-Imran :85). Aya hii inaonyesha dini zilizobuniwa na watu. Bainisha dini hizo
b) Elezea hatua za kushuka Qur’an
5. a) Eleza kwa kutoa hoja mbili(02) kwa nini ni muhimu kufauta sunnah ya Mtume (S.A.W) katika maisha ya kila siku
b) wewe kama mtaalamu wa sunnah na hadithi elezea tofauti tatu(03) zilizopo baina ya sunnah na hadithi
6.a) Suratul-faatihah imepewa majina mbalimbali kutokana na maudhui yanayopatikana ndani yake. Bainisha Majina Matano ya suratul-faatiha
b) Wanafunzi wengi wanaosoma elimu ya dini ya kiislamu hawaelewi uhusiano uliopo baina ya elimu ya dini ya kiislamu na masomo mengine. Wewe kama mtaalamu wa kidato cha kwanza wawafafanulie uhusiano uliopo kwa hoja tatu
c) Elezea sababu mbili zinazoruhusiwa na uislamu kwa mtu kutayammamu
7.a) Mtume (S.A.W) ametufahamisha kuwa uislamu umejengwa juu ya nguzo tano . Fafanua nguzo hizo kwa mpangilio.
b) Wakati ukiwa shule mzazi wako alipaiga simu kwa Mwalimu wako na kumtaarifu kuwa Jirani yenu amafarki na hakuna mwenye elimu ya kuosha maiti isipokuwa wewe mtaani kwenu, mama akaomba ruhusa ya wewe Kwenda kuosha maiti. Elezea hatua kwa hatua namna utakavyomuosha maiti huyo.
8.a) Bainisha makundi ya najisi na mifano yake
b) Bainisha namna ya kujitwaharisha kwa kila kindi
c) Elezea maana ya hedhi, nifasi na janaba
9. a) Shirki imegawanyika katika makundi mawaili. Bainisha makundi hayo
b) Mtu anae mshirikisha Allah (S.W) atajidhihirisha maeneo matatu. Fafanua maeneo hayo
SEHEMU C (ALAMA 15)
Jibu swali la kumi (10)
10. Juma hatekelezi ibada ya swala kwa sababu anasumbuliwa na maradhi mbalimbali. Kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza, toa elimu kwa Juma namna gani mgonjwa anaweza kutekeleza swala za faradhi.
FORM ONE EDK EXAM SERIES 284
FORM ONE EDK EXAM SERIES 284